Judith Ferdinand, Mwanza
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limehimizwa kuwa makini na kufanya maamuzi sahihi katika michezo iliyosalia katika ligi daraja la kwanza ili kuhakikisha timu itakayopanda ligi kuu ni iliyo na sifa.
Hayo yamesemwa na kocha mkuu wa timu ya Alliance Sports Club ya Jijini Mwanza, Mbwana Makata alipokuwa akizungumza BMG wakati mazoezi katika uwanja mkongwe wa Nyamagana.
“Sisi Alliance tunaimani timu yetu ni bora na itafikia mafanikio,hivyo tunaomba TFF na Bodi ya Ligi, katika michezo hii ya mwisho,waweze kuwa makini na maamuzi pamoja na waamuzi wachezeshe michezo kwa kufuata sheria na kanuni za mpira, ili kuhakikisha timu inayopanda ligi kuu ni yenye sifa,”alisema Makata.
Pia alisema timu hiyo inaongoza kwenye kundi lao la C kwa pointi 19,ikifatiwa na Dodoma FC 18 na Biashara ya Musoma ikiwa na pointi 17,hivyo ushindani katika kindi hilo ni mkubwa kwani timu zote zinahitaji ushindi na anaimani timu yao ni bora, itaweza kufikia mafanikio sambamba na kufanya vizuri.
Hata hivyo,aliwaomba mashabiki kushabikia timu hiyo katika mechi zao ziliosalia ambapo mchezo unafuatia watakutana na Dodoma FC katika uwanja wa Mpwapwa mkoani Dodoma desemba mwishoni,sambamba na kutoa sapoti ili kuweza kuwapa hamasa na nguvu na hatimaye kufanya vizuri.
Kwa upande wake Nahodha wa Alliance Hance Masoud alisema wanafuata maelekezo kutoka kwa walimu wao, ili kufanya vizuri na kujipanga vyema katika mchezo wao na Dodoma FC na mingine iliyosalia.
Masoud alisema,ni kweli kundi C ni gumu na kila mtu anatoa macho kwa sababu anahitaji ushindi na hatimaye kufuzu kuingia ligi kuu, kwani kujiandaa na kujipanga vyema husaidia kufanya vema kwenye mechi.
0 comments:
Post a Comment