METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 19, 2017

Bodi Mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa TFC yazinduliwa Jijini Dar

 Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), (hawapo pichani), wakati akiizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi.
 Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa, Egid Mbofu, akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Mkuu wa TFC, Salum Mkumba.
 Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa bize kuchukua maagizo ya Waziri Mwijage.
 Waziri Mwijage akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.
 Hapa ni kalamu zikizungumza katika uzinduzi huo wakati Waziri Mwijage alipokuwa akiipa majukumu bodi hiyo mpya ya TFC.
 Uzinduzi ukiendelea.
Waziri Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.

Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.

Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo,  Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.

Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.

“Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi”, alisema Waziri Mwijage.

Aliongeza kusema kwamba, mazingira ya sasa ya kilimo kwa Tanzania, yanahitaji umakini katika uagizaji wa mbolea zinazotumiwa na wakulima wengi ambao malengo yao ni kupata faida, lakini wamekuwa wakiangushwa na baadhi ya wafanyaviashara wanaoagiza mbolea feki.

TFC ni mtoto wa serikal, hivyo nimeagizwa na mheshimiwa Rais, kuwaonoa hofu na kwamba tunahitaji kuiongezea uwezo ili Taifa liweze kufikia malengo ya uzalishaji mkubwa wa chakula pamoja na mazao mengine yanayohitajika kama malghafi katika viwanda.

Kwa upande wake Profesa Mbofu, alimshukuru Waziri Mwijage na kumuahidi kwamba, wako tayari kwa kazi hiyo lakini pia akasema wamfikishie Rais shukrani zao kwa uaminifu wake kwao.

“Ninaomba kwa niaba ya wajumbe wa bodi hii, menejimenti ya TFC kukushukuru kwa kazi hii nzuri na maagizo yako yote kwetu, tunakuahidi kuifanya kazi hii kwa uaminifu na uadilofu mkubwa na tutaendelea kuomba ushauri wako kila tunapohitaji kufanya hivyo kama njia ya kupata miongozo zaidi,” alisema Profesa Mbofu.

Meneja Mkuu (GM),  Salum Mkumba, alimhakikishia Waziri Mwijage, kwamba TFC iko tayari kwa mabadiliko ya aina yeyote na wafanyakazi wako tayari kwa kusimamia maagizo kwa ajili ya kuendana na Tanzania ya Viwanda kulingana na sera na miongozo ya serikali ya awamu ya tano.
Pia GM Mkumba, alisema TFC ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo chini ya wizara ya Viwabda na Uwekezaji, ambazo tayari zilianzisha mabaraza ya wafanyakazi kwa ajili ya kuwashirikisha wafanyakazi na kuwajengea uwezo wa kushauri kasi ya maendeleo kwenye kampuni hiyo ya umma.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com