]Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi na baadhi ya wananchi ambao wameathirika kutokana na maji Hayo kwenye maeneo ya mashamba.
(PICHA NA JOEL MADUKA)
Ekari 270 za mashamba ya wakulima kwenye kijiji cha Ziwani Kata ya
Nyarugusu Wilayani Geita zimeathiriwa na Sumu iliyotoka kwenye Bwawa la
kuhifadhia Kemikali lililopasuka kingo zake na maji kusambaa kwenye mashamba
hayo.
Hali hiyo imemlazimu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Bw Kangi Lugola kuitaka kampuni ya Madini ya Nyarugusu
inayohusika na suala hilo kuwalipa fidia wananchi 57 ambao mazao yao
yameathirika.
Awali Bw Lugola aliagiza muwekezaji huyo akamatwe kutokana na kile
alichodai kuwa ni uvunjifu wa sheria za utunzaji wa mazingira mgodini hapo na
kwamba uongozi wa mgodi huo ulimzuia Afisa Mazingira wa Wilaya ya Geita Bi
Hellen Eustace kutekeleza majukumu yake baada ya kufika mgodini hapo kukagua
namna wanavyozingatia utunzaji mazingira
Bw Kangi alisema Mwekezaji haruhusiwi kuendelea na shughuli
anazozifanya na kufunga mgodi huo hadi watakapotekeleza mambo waliyoelekezwa
Mkurugenzi wa Nyarugusu Mine Company Bw Fred Masanja amesema
kusimamishwa kwa shughuli zao kunaweza kuathiri ytendaji wao kwa kuwa Tani Laki
moja na 20 hawataweza kuzizalisha na hivyo watapata hasara ya zaidi ya Sh
Milioni 600 hadi 700
|
0 comments:
Post a Comment