METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, December 17, 2017

MASHINDANO YA IKUNGI ELIMU CUP YAFIKA UKOMO WILAYANI IKUNGI, DC MTATURU APONGEZWA KUANZISHA MFUKO WA ELIMU

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akifatilia kwa makini mchuano mkali baina ya timu ya Mampando Fc na Matongo Fc, Mchezo uliomalizika kwa Timu ya Mampando Fc kuibuka na ushindi wa goli 2-0, Juzi 16 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi zawadi kwa timu zilizoshiriki mashindano ya "IKUNGI ELIMU CUP 2017" baina ya timu ya Mampando Fc na Matongo Fc, Mchezo uliomalizika kwa Timu ya Mampando Fc kuibuka na ushindi wa goli 2-0, Juzi 16 Disemba 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi zawadi kwa timu zilizoshiriki mashindano ya "IKUNGI ELIMU CUP 2017" baina ya timu ya Mampando Fc na Matongo Fc, Mchezo uliomalizika kwa Timu ya Mampando Fc kuibuka na ushindi wa goli 2-0, Juzi 16 Disemba 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi zawadi kwa timu zilizoshiriki mashindano ya "IKUNGI ELIMU CUP 2017" baina ya timu ya Mampando Fc na Matongo Fc, Mchezo uliomalizika kwa Timu ya Mampando Fc kuibuka na ushindi wa goli 2-0, Juzi 16 Disemba 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali "IKUNGI ELIMU CUP 2017" baina ya timu ya Mampando Fc na Matongo Fc, Mchezo uliomalizika kwa Timu ya Mampando Fc kuibuka na ushindi wa goli 2-0, Juzi 16 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog

Mashindano ya "Ikungi Elimu Cup mwaka 2017" juzi 16 Disemba 2017 yalifikia ukomo Wilayani Ikungi Mkoani Singida ambapo timu ya Mampando Fc ndiyo iliyoibuka kidedea na kunyakua kombe la "Ikungi Elimu Cup 2017" kwa kuibamiza bila huruma timu ya Matongo Fc kwa jumla ya mabao 2-0.

Michuano hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na kuendeshwa na Chama cha Soka wilayani Ikungi, ilizinduliwa Agosti 19, 2017 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi huku ikizikutanisha timu 69 Wilayani humo.

Akizungumza katika kilele cha Mashindano hayo kilichofikia ukomobkatika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa mashindano hayo yalianzishwa kwa lengo mahususi la kuutangaza na kuutambulisha mfuko wa elimu wa Wilaya ambapo miongoni mwa mafanikio yake ni kuchaguliwa vijana 30 watakaoingia kambini mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka 2018 ili ipatikane timu imara ya Wilaya itakayoshiriki mashindano mbalimbali katika 
Ngazi ya Mkoa, Kanda na Taifa.

Alisema kuwa mashindano hayo pia yamekuwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za elimu wilayani Ikungi ikiwemo ujenzi wa Madarasa, Maabara, Nyumba za waalimu pamoja na vyoo.

Pamoja na Wazo hilo kuibuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Mtaturu ambaye ni mlezi wa mfuko wa elimu Wilaya ulioanzishwa kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa changamoto za kielimu wilayani humo pia umeongeza chachu na hamasa katika Michezo ikiwa ni pamoja na utambuzi wa vipaji mbalimbali kwa vijana.

Wakati wa kusoma taarifa ya mashindano hayo katibu wa chama cha mpira Wilaya Ndg Mwendwa alisema mashindano hayo yalianzia ngazi ya Vitongoji, Vijiji, Kata,Tarafa na hatimaye katika wilaya.

Mhe Mtaturu ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo Agosti 29, 2017 mbele ya wananchi na wachezaji ya kugawa vifaa vya michezo kwa timu zote 69 ambapo walijipatia jezi na mpira.

Katika mashindano hayo Mshindi wa kwanza ambayo ni timu ya Mampando Fc amekabidhiwa zawadi ya Kombe, Seti ya jezi, Mpira na kitita cha Shilingi milioni 1.

Mshindi wa pili timu ya Matongo Fc imepewa mpira na shilingi 400,000, Mshindi wa tatu timu ya Masutianga Fc imekabidhiwa kitita cha Shilingi 300,000 ambapo timu ya Ikungi Fc imekabidhiwa shilingi 50,000 kwa kushika nafasi ya nne huku Mshindi wa tano Masweya Fc akikabidhiwa shilingi 50,000.

Aidha, kulikuwa na zawadi  ya Mchezaji bora, Mchezaji mwenye nidhamu, Mfungaji bora na Goalkeeper bora ambapo kila mmoja alipatiwa viatu maalumu vya kuchezea mpira wa miguu (njumu)

Kwa upande wa Uongozi wa Cha mpira wa Miguu Wilaya ya Ikungi (IDFA), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, na Mwenyekiti wa mfuko wa elimu wa Wilaya hiyo wamempongeza na kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kubuni na kuanzisha mashindano ya "IKUNGI ELIMU CUP 2017" ambayo yamekamilika huku yakiwa yamewaunganisha vijana na wananchi katika Umoja na mshikamano.

Katika hotuba yake Mkuu huyo wa Wilaya aliwapongeza viongozi wote na timu zote zilizoshiriki ligi hiyo kwani bila wao kusingekuwa na mafanikio yenye tija.

Mhe Mtaturu aliwahakikishia wananchi kuwa mashindano hayo yataendelea kwa miaka mitatu mfululizo ili kutekeleza mpango mkakati wa mfuko wa elimu wa Wilaya.

"Ndugu zangu huu ni mwanzo wa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye shule zetu ili kuongeza ufaulu na kuboresha elimu ya watoto wetu na hii ni hatua muhimu katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kuinua ubora wa elimu nchini.

Sambamba na hayo pia mpaka sasa mfuko umefanikiwa kupokea Jumla ya mabati 100, mifuko ya Saruji 294, mamlaka ya elimu Tanzania (TEA) wamechangia Milioni 141,000,000/-kujenga nyumba 6 za walimu (ambazo zitajengwa kwenye shule ya Sekondari Lighwa ambayo inamazingira magumu), Milioni 45,000,000/- kusaidia kutatua changamoto za shule ya msingi mchanganyiko Ikungi na wananchi wameshafyatua matofali yapatayo 79,000.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com