
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philipo Mpango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati
za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina
SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Hazina SACCOS, Aliko
Mwaiteleka,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati
za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina
SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma


Sehemu ya wanachama wakifatilia
uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa
Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika
katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philipo Mpango,Hati yake wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za
ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS,
tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mwanachama akipokea hati yake
katika ni waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akishuhudia
tukio hilo wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo
la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio
lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philipo Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanachama mara baada ya
kuzindua hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa
Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika
katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
…………………….
Na.Alex Sonna, Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philipo Mpango, amezitaka benki na taasisi nyingine za kifedha
kuangalia upya namna ya kukokotoa viwango vya riba wanavyoviweka katika
mikopo wanayoitoa kwani ni viwango vya juu na haziwanufaishi wanaokopa
na kuwa sio msaada tena.
Pia ameitaka Banki kuu ya Tanzania
BOT kuzifanyia utafiti benki zote na taasisi za kifedha kama
zinazingatia vigezo hasa katika riba wanazotoza kwa wanachama wao na
zinafuata utaratibu uliowekwa.
Waziri Dkt. Mpango, ameyasema hayo
leo Jijini Dodoma wakati akizindua hafla ya ugawaji hati za ardhi,
eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio
lililofanyika katika ukumbi wa Hazina Dodoma.
Dkt. Mpango amesema amekutana na
benki moja ambayo inatoa mikopo kwa watumishi kwa riba ya asilimia 32,
na alipowauliza na wao wakasema wanachukua mikopo hiyo katika benki
nyingine kwa riba ya asilimia 20, jambo ambalo riba hiyo ni kubwa sana.
“Ni jana tu nimekutana na benki
hiyo na kukuta inatoa riba kwa asilimia 32 na nilipowadodosa wakanijibu
na wao wanachukua mikopo hiyo benki nyingine kwa asilimia 20, lakini hii
ya asilimia 20 bado ni kubwa sana, niitake benki kuu kutafiti hivi
viwango vya riba kwa mabenki yote na taasisi zote za kifedha” amesema
Dkt Mpango.
Aidha amekipongeza kikundi cha
Hazina SACCOS, kwa kupima maeneo na kupata viwanja kwa ajiri ya
wanachama wake, kwani jambo hilo ni kuunga mkono serikali katika
kuendeleza makao makuu ya nchi na kuendeleza Jiji la Dodoma.
Pia amewataka watumishi wa
serikali kuchangamkia fulsa kwa kujiunga na chama hicho cha ushirika
hazina SACCOS, ili kama watumishi wa serikali waweze kunufaika na
mikopo ya bei nafuu inayotolewa na hazina SACCOS, na kukitaka kikundi
hicho kuzingatia maadili na kuepuka ubadhilifu.
Waziri Dkt Mpango amemtaka mlezi
wa hazina SACCOS, ambaye ni katibu mkuu wa Wizara hiyo, Dotto James,
kuketi meza moja na Mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Tanzania(TRL)
Masanja Kadogosa, kama wamemaliza suala la kupima eneo yanayopitiwa na
reli ya kisasa ili watumishi wenye viwanja maeneo hayo waanze
kuviendeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Hazina SACCOS, Aliko Mwaiteleka, amesema chama hicho kilianzishwa mwaka
1973, na waliokuwa wafanya kazi wa Wizara ya Fedha, na baadaye kusambaa,
na kina wanachama zaidi ya elfu tano mia sita(5600), na kinajihusisha
na utoaji wa mikopo ya bei nafuu na kina akiba ya shilingi bilioni
nane(8).
0 comments:
Post a Comment