Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, akiwahutubia wanafunzi
wa chuo cha Rungemba pomoja na wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya
maadili na haki za binadamu.
Sehemu ya Wanachuo wa Chuo cha Rungemba pamoja na Wananchi wakisikiliza
hotuba ya mgeni wa heshima.
Mkuu Takukuru Wilaya ya Mufindi Bw. Orest Mushi, akiwasilisha mada.
Na Afisa Habari Mufindi
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh.
Jamhuri William amesema, endapo Ofisi za Umma hazitodhibiti
ipasavyo mifumo na urasimu uliowekwa kwenye Ofisi za Serikali,
masuala hayo yanaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kuendelea kukua kwa tatizo la
rushwa katika ofisi hizo.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa
kauli hiyo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu,
iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo
Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
Mh. Jamhuri amesema, urasimu
uliyowekwa kwa nia njema ya kuthibiti utendaji kazi ukitumiwa vibaya, unaweza
kuwa chanzo cha rushwa, hivyo akatoa rai kwa taasisi zote za umma kuhakikisha
zinazingatia suala la kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja na kusisitiza kuwa,
hiyo ni moja kati ya njia kuu za kuondoa suala la rushwa katika Ofisi za umma.
Awali Mkuu wa taasisi ya
kuzui na kupambana na rushwa Wilayani Mufindi bw. Orest Mushi, ametanabaisha
kuwa tafiti za hivi karibuni zinazoonesha kupungua kwa rushwa
nchini, zinatokana na utashi wa kisiasa uliopo, chini ya Rais John Pombe
Magufuli, huku akibainisha malengo ya maadhimisho hayo, kuwa ni pamoja
na kuiwezesha Serikali kufuatilia na kufahamu hali ya rushwa nchini,
kubainisha madhara ya rushwa na kutambua umuhimu wa kuendelea kupambana nayo,
kutambua changamoto za mapambano dhidi ya rushwa, kuweka mikakati ya kupambana
na rushwa, sanajari na kuisaidia nchi kutathimini ushiriki
wake dhidi ya mapamabano ya rushwa kimataifa.
Mwaka 2005 serikali iliamua
kwamba maadhimisho haya yawe yanafanyika disemba 10 ambapo, nchi yetu huungana
na mataifa mengine duniani kuiadhimisha kama siku ya maadili na haki za
binadamu. Kaulimbiu ya mwaka huu ni wajibika piga vita rushwa, zingatia
maadili na haki za binadamu, kuelekea uchumi wa kati.
0 comments:
Post a Comment