WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, Viongozi wa Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw.
Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu,
Tuangoma Jijini Dar es Salaam.
Bw. Msulwa amefariki dunia juzi (Alhamisi, Novemba 16, 2017)
katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika maombolezo hayo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.
Waziri Mkuu amesema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi na mwenye
ushirikiano mzuri na wenzake, ambapo Novemba 12, 2017 alipokea barua kutoka CWT
iliyosainiwa na marehemu akimualika kushiriki kwenye shughuli za chama.
“Wote tumeguswa na msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu
wa Chama cha Walimu Tanzania tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa
kila mmoja. Alikuwa na tabia njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema
aliyotuachia”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi
Mungu ailaze roho yake mahali pema. Nawaomba wanafamilia, mke wa marehemu na
watoto kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na
mpendwa wetu.”
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar
es Salaam
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P.
980,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 16, 2017.
0 comments:
Post a Comment