Umoja wa Mataifa kupitia Umoja wa Vijana (YUNA) umetoa tuzo kwa Taasisi na watu binafsi wenye mchango mkubwa katika maisha ya watu barani Afrika.
Kupitia tuzo hizo zinazotambulika kama PAHA, kituo cha Televisheni cha Clouds kimetambuliwa kama kituo bora cha Runinga kwa mwaka 20117.
Hiyo ni kutokana na kurusha maudhui yanayomulika maisha ya watu na kutoa tumaini kwao kupitia vipindi na kampeni mbalimbali kama vile...
(#IshiNaMimi #Kipepeo #MalkiaWaNguvu #RudishaTabasamuMiaMoyo na nyinginezo)
Baada ya kupokea tuzo hiyo ya heshima Kampuni ya Clouds Media Group imeishukuru YUNA pamoja na umoja na umoja wa mataifa kutokana na Utambuzi huo.
Sambamba na hilo Clouds Tv imewashukuru Watanzania Kwa kuendelea Kuwaamini na Kuwachagua.
" Tunaahidi kuendelea kuwatumikia kwa moyo na nguvu zaidi kwani tulishakula kiapo cha kuwa Taasisi ya watu" sehemu ya taarifa hiyo ilieleza.
(#RedioYaWatu #ThePeoplesStation)
#TunakufunguliaDuniaKuwaUnachotaka
0 comments:
Post a Comment