WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na
kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Meja Jenerali
Issa Suleiman Nassoro na Balozi Abdulrahman Kaniki wa Zambia, ambapo amewataka
wakaimarishe mahusiano baina ya nchi zote mbili.
Amekutana na Mabalozi hao Balozi leo
(Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Barabara ya
Reli na Mahakama mijini Dodoma na kuwasisitiza wakaboreshe shughuli za Kidiplomasia
kati ya Tanzania na nchi za Misri na Zambia.
Pia Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao
wakahakikishe wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima
Kilimanjaro, mbuga za wanyama, fukwe pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo
nchini hususan katika sekta ya viwanda.
Amesema licha ya kutangaza fursa za
uwekezaji na vivutio vya utalii pamoja na kuboresha biashara baina ya Tanzania
na nchi za Misri na Zambia pia wakawashawishi wawekezaji waje wawekeze katika sekta
mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanda.
Waziri Mkuu amesema
Tanzania ni nchi salama yenye amani na utulivu wa kisiasa, pia Serikali imeweka
mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha wawekezaji watakaokuja
kuwekeza nchini kupata tija.
Pia Waziri Mkuu
amewataka Mabalozi hao wahakikishe wanakwenda kutafuta masoko ya bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa nchini.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka Mabalozi
hao kwenda kukutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio kwenye nchi
hizo na kuwasisitiza waishi kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia wawaunganishe
pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini.
Kwa upande wao Mabalozi hao wamesema watahakikisha
wanayafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa na Waziri Mkuu ikiwa ni pamoja na
kwenda kutafuta wawekezaji ili wawe kuwekeza katika sekta ya viwanda na
kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P.
980,
DODOMA.
ALHAMISI, NOVEMBA 16, 2017.
0 comments:
Post a Comment