Diwani wa Kata ya Mgusu,akionesha moja kati maeneo ambayo shule hiyo inatarajia kujengwa. |
Vifaa vya ujenzi yakiwemo Mawe na Kokote vikiwa kwenye eneo la ujenzi wa shule ya sekondari. |
Diwani wa Kata ya Mgusu,Pastory Ruhusa akiwa kwenye eneo la ujenzi na akizungumzia hatua ya ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ya kata. |
Wakazi wa Kata ya Mgusu wilayani Geita wameanza kujenga msingi wa shule ya sekondari ya kata hiyo ili kupunguza tatizo la wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo.
Diwani wa kata hiyo Bw
Pastory Ruhusa alisema wananchi wamechangia ujenzi huo ili kuwanusuru wanafunzi
wanaolazimika kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.
“Wanafunzi wa kata hii
wanapata shida sana wanatembea umbali wa kilomita 20 kufuata masomo na muda
mwingine kutoka hapa kwenda shule ya sekondari ya shantamaini ni mbali sanaa na
usafiri ni washida ndio maana tumeonelea mimi nikiwa kama diwani na wananchi wa
kata hii ya Mgusu tuchangishane ili tuweze kujenga shule ambayo tunafikiria
kama Mungu itampendeza mwakani waanze kusomea hapa wale ambao wamemaliza
mtihani wa shule ya msingi mwaka huu”Alisema Diwani
Baadhi ya wazazi Bi Naomi
Barubaru na Bw Mussa Ngozi walisema tatizo la umbali na kukosekana usafiri maalum
wa wanafunzi limesababisha waanze ujenzi huo.
“Ndugu mwandishi kiukweli
inatuumiza sana sisi kama wazazi kuendelea kuona watoto wetu wanashindwa
kutumiza ndoto zao kutokana tu na umbali wa kufuata masomo tumeonelea ni bora
tuanze ujenzi maana hapa tunamgodi wa GGM lakini hauna manufaa yoyote kwenye
kata pamoja na kwamba wanafanya shughuli za uzalishaji dhahabu tunasikia tu
wanatoa misaada Arusha lakini maeneo ambayo wanapatia hizo mali wananchi tupo
hoii”Alisema Mzee Ngozi.
“Mabinti zetu wamekuwa
wakikutana na shida sana pindi wanapokwenda shuleni wengine wameshindwa
kumaliza kutokana na kupata mimba kwasababu tu ya umbali tunadhani kukamilika
kwa shule hii itasaidia wanafunzi kusoma karibu na makazi yao”Alisema Bi,Naomi.
Meneja mwandamizi wa
masuala ya jamii kwenye Mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM Bw Manase Ndoroma alisema
mgodi huo umetenga fedha za kujenga jingo la utawala kwenye shule hiyo kwa
mwaka 2018 baada ya mwaka jana kuwapa wananchi hao Sh Milioni 15.
Wanafunzi hao wanalazimika
kutembea umbali wa Kilomita 25 Mgusu kwenda shule ya sekondari ya Mtakuja
kufuata masomo .
0 comments:
Post a Comment