Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa klabu ya Azam
umepanga kufanya usajili wa mchezaji mmoja wa kigeni kutoka katika nchi
za Ghana na Zambia ambapo wanatarajia kushusha wawili ili kupata
straika mmoja kati yai atakayemrithi Yahaya Mohamed.
Mapema mwezi huu, uongozi wa timu hiyo ulivunja mkataba na
mshambuliaji wake Yahaya Mohammed ukiwa unakaribia mwaka mmoja tangu
alipojiunga na timu hiyo kwa kile kinachodaiwa ni kushindwa kuonyesha
kiwango kizuri tangu ajiunge na timu hiyo.
Azam FC imefikia makubaliano ya pamoja na mchezaji huyo
raia wa Ghana na tayari wamemkabidhi barua ya kumruhusu kuondoka klabuni
hapo.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd amesema leo mjini
Dar es Salaam kwamba, wiki ijayo uongozi wa Azam utamwagiza wakala wao
wa kufuatilia wachezaji wa nje ya nchini kwa ajili kwenda Ghana na
Zambia kufuatiliwa wachezaji hao na iwapo ataridhishwa na mmoja kati yao
basi atarudi naye kwa ajili ya kujiunga nao.
“Baada ya kuachana na straika wetu Yahya Mohamed, kocha
amependekeza kati ya wachezaji wawili kutoka Ghana na Zambia ili aweze
kumpata mmoja wao kwa ajili ya kuziba nafasi ya huyo
aliyeondoka,”alisema.
Wakati huo huo, Jafari alisema, kikosi cha Azam
kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda Njombe kwa ajili ya mechi yao dhidi
ya Njombe Mji, mchezo wa raundi ya 10 wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa
Jumamosi hii kwenye uwanja wa Sabasaba.
Alisema, kikosi cha wachezaji 22 akiwemo na Stephane Kingue
ambaye alikuwa majeruhi, kinatarajiwa kuondoka kikiwa pamoja na
viongozi wa benchi za ufundi kwa ajili ya kwenda mjini humo.
“Timu inaondoka mapema kwa ajili
ya kwenda kuzoea mazingira ya baridi na Njombe ikiwa ni pamoja na
kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa wenyeji Njombe Mji kwenye
mchezo huo,” alisema Jaffar.
0 comments:
Post a Comment