Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.
Kwa upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara.
“Najisikia furaha sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono. Tumekuwa na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa tukiendelea kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi makunwa sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa Afrika kwa ujumla.
Tunaamini Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua na kulinda utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni wake ndani ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie Kaarstad.
Balozi huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana mahala pamoja kufurahia.
Aidha, Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud amebainisha kuwa, msimu wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari wametangaza listi ya wasanii na vikundi ambapo jumla ya vikundi 20 kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC, Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan, Gambia.
Pia vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland.
Katika vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha uwezo wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia 100 ‘live’ kwa siku nne mfululizo.
Pia kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa ndani na nje ambao watapata kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza sanaa na masoko ya muziki wao.
Na Andrew Chale-MO BLOG, Dar e Salaam.
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud akizungumza katika tukio hilo. Kushoto ni Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa Norway na Busara Promotions.
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati walizotiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017.
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakijibu maswali kutoka kwa wanahabari (Hawapo pichani) mapema leo Novemba 2, 2017. ( PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).
0 comments:
Post a Comment