METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, November 5, 2017

SHAKA AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA BOMAMBUZI-MOSHI MJINI

*Baadhi ya aliyoyasema Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka  (MNEC) wakati  akizindua rasmi na kumnadi mgombea wa  udiwani kata ya Bomambuzi.*

"April 2016 nilifika  kuzungumza nanyi katika viwanja hivi kukiwa  na mvua kama Leo, nikawambia  nitarudi kuja kumnadi mgombea wa CCM na Leo nimerudi, sasa Leo nawambia  tena inshallah nitarudi kuja kuwapongeza kwa kumchagua  mgombea wa CCM katika uchaguzi wa November 2017" Shaka

" Hakuna na hatatokea  wa kuzuwia ushindi wa CCM Boma mbuzi tutashinda kwa amani, kwa haki, usawa na demokrasia na Juma Raibu ndie diwani wenu hapa kwa mapenzi  ya mungu" Shaka

"Wananchi watahadharini wagombea wa upinzani kwani vyama vyao  vimevamiwa na viongozi wasaka  madaraka huku wakikosa sifa ya kupigania  maendeleo na kukosa ujasiri wa kutetea maslahi ya umma"  Shaka

*Wananchi wa Kata ya Bomambuzi  wakataeni  wagombea  hao na vyama vyao kwa kuwanyima kura na kumpa kura Juma Rahibu wa CCM ". 

"Wananchi hawapaswi kuviunga mkono vyama vya upinzani  kwakuwa havina sera wala ajenda ya kupigania maendeleo pia hawana uchungu na si watetezi wa rasilimali za Taifa" Shaka

"Wananchi wa Kata ya Bomambuzi msikubali  kughilibiwa na Chadema kwani  chama hicho  ni  zizi la kuhifadhi mafisadi na tunavishauri  vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa hao wanaotumia siasa  za ukabila,  ukanda, udini na rushwa" Shaka

"Nazumgumza na watanzania kupitia  wakazi wa Bomambuzi nawatahadharisha kukiogopa chadema kama ukoma.Viongozi wake wameanza kupita mitaani wakinadi ukabila na udini mambo ambayo ni kinyume na matakwa ya kisheria na kikatiba ." Shaka  

"Hao ndio aina ya viongozi walioko chadema.Wakati watu wakitafuna miwa , chadema wameamua kuokota maganda na kuona wamepata chumo huku kikikubali kuwa  zizi la  mafisadi " Shaka

"Wananchi mchagueni Juma Raibu awe diwani wenu, ni mwanasiasa  asiyeyumba na msimamo, mzalendo na hatawatupa wana Bomambuzi au kuihama CCM kwa tamaa ya  madaraka  " Shaka  

'Nawaasa baadhi ya viongozi  wa CCM  kuacha kufanya udalali  na biashara katika siasa kwa kujipatia fedha  badala yake wajenge uaminifu na kuwa wazalendo kwa chama na kukipatia ushindi" Shaka

"Binadamu  hujifunza kwa makosa. Makosa ya mwaka 2015 kuchagua wagombea wa chadema  yasirudie.Hawana uwezo wa kuwaletea maendeleo na huduma wananchi" Shaka

"Aina  ya viongozi wao ni dhaifu na wabaishaji mchaguni Juma aje kuungana na Rais magufuli katika kuleta maendeleo endelevu ya bomambozi" Shaka 

Mapema Kaimu katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka aliwapokea wanachama zaidi ya 60 waliohama chadema na kujiunga na CCm.

*Aliyoyasema mgombea wa CCM Juma Raibu wakati akiomba kura.*

"Nitazitumia sera za ccm , ilani yake ya uchaguzi na utendaji  wa serikali ya awamu ya tano  kuwaletea  maendeleo katika Kata hii ikiwa nitaachaguliwa " Juma

"Uamuzi wa kumchagua mgombea  wa upinzani ambaye hana ukaribu na Waziri dhamana, hajuani na Waziri Mkuu, Makamu Rais na Rais wa nchi ni kuharibu kura kwani mgombea wa Chadema hawezi kuzungumza na mkuu wa nchi kama wafanyavyo viongozi wa CCM" Juma. 

"Nimezaliwa Bomambuzi, nimekulia hapa, watoto hapa na familia, nitaendelea  kuishi hapa sitaondoka  labda kwa kufa ni chagueni niwatumikie" Juma

Nawashkuru wote walionisimamia na kuhakikisha haki inatendeka na Leo tunakwenda  kuikomboa kata yetu mikono mwa wababaishaji na kuirudisha  kwa CCM " Juma

" Nitasimamia uboreshaji wa huduma  za afya, elimu, miundo mbinu  ya barabara za ndani na nitakuwa kiungo muhimu baina  yenu na serikali" Juma

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com