Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula leo amemnadi na kumwombea Kura mgombea wa udiwani Kata ya Mhandu kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndugu SIMA CONSTANTINE SIMA baada ya kutangazwa kwa uchaguzi mdogo unaoendelea maeneo tofauti tofauti nchini
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Mhandu Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa kata ya Mhandu kumpa Kura za NDIO mgombea huyo ili kujiletea maendeleo kwa kuwa Ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi hivyo kuchagua chama tofauti ni kukataa maendeleo kwa hiari yao wenyewe kwani hatakuwa na pahala pa kupeleka shida za wananchi na hakutakuwa na Ilani atakayotekeleza kutoka kwenye chama chake tofauti na CCM huku akiwahakikishia kumaliza kabisa changamoto zao za Ardhi zinazowakabili
‘… Ndugu zangu mie pia natokea wizara ya Ardhi na kilio chenu nimekisikia tangu jana, Nichagulieni Diwani Mhe SIMA tushirikiane na mbunge wenu na mara zote mmekuwa mkimsikia bungeni akinilalamikia juu ya changamoto za zoezi la Urasimishaji na suala la bei ya hati sasa ili tuweze kumaliza changamoto hizi hakikisheni mnanichagulia Ndugu SIMA na niwaambie Wizara yangu imeshaanza kulifanyia kazi suala hili …’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewahakikishia Ulinzi na Usalama wananchi wa kata ya Mhandu na kuwataka kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula amewataka wananchi wa kata ya Mhandu kumchagua Ndugu SIMA CONSTANTINE SIMA ili aweze kushirikiana nae katika kuwaletea maendeleo huku akitaja miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili tangu Serikali ya awamu ya Tano kuingia madarakani
Akihitimisha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko amewataka wananchi hao kutofanya makosa na siku ya uchaguzi kukipa Kura za NDIO Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka wapinzani kuacha kudandia gari kwa mbele na kuongopea Umma ya kwamba hakuna shughuli zozote za maendeleo zinazofanyika
Mkutano huo wa Kampeni pia ulihudhuriwa na Mbunge wa Viti maalumu kupitia kundi la Vijana wa CCM Mkoa Mwanza Mhe Maria Kangoye, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe James Bwire, Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana, madiwani wa kata za wilaya ya Nyamagana, makatibu wa Jumuiya na viongozi wa chama cha mapinduzi kutoka kata tofauti tofauti
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
24.11.2017
0 comments:
Post a Comment