METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, November 24, 2017

MHE DKT ANGELINE MABULA MGENI RASMI MIAKA 10 YA CHUO CHA CBE MWANZA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula ameshiriki sherehe za kutimiza miaka Kumi tangu kuanzishwa kwa Tawi la Chuo cha Biashara nchini CBE jijini Mwanza zilizoenda sambamba na Uzinduzi wa majengo ya kampasi hiyo iliyopo eneo la Kangaye wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza

Akizungumza katika sherehe hizo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kushukuru kwa kualikwa kama mgeni rasmi amefurahishwa na ujio wa chuo hicho ndani ya jimbo lake na kuwataka wananchi kuona ujio huo kama fursa katika kujikwamua kiuchumi sanjari na kuwataka kulinda eneo lao ili kujiepusha na uvamizi lengo likiwa ni kufikia Sera ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda

‘… Kwakweli nawashukuru sana kwa kazi kubwa ya kuchochea maendeleo hasa kwa miaka hii kumi ya uwepo wenu hapa Kanda ya Ziwa ila niwashauri tu kwakuwa mmewekeza kwenye Ardhi na mie ndiko ninapotokea huko  kama tunavyosema ardhi ni mtaji,  hata kama hautawekeza leo, kile kitendo cha kuwa na ardhi kubwa kinapanua fursa ya uwepo wa mambo mengine ukizingatia hichi ni chuo cha biashara …’ Amesema
Aidha mbali na kuwapongeza kwa kutimiza miaka 10 ya mafanikio amewataka wananchi wanaoishi jirani na chuo hicho kutoa ushirikiano kwa uongozi wa chuo na wanafunzi wake ili kutoa fursa ya kujiletea maendeleo baina yao wenyewe

Akimkaribisha mgeni rasmi mwakilishi kutoka wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji amesema kuwa wizara ina mpango kababe wa kuwatumia wataalamu kutoka Chuo cha CBE ili kutoa fursa ya watu kujifunza zaidi juu ya Tanzania ya Viwandana sambamaba na kuwa na mitaala inayoendana na wakati

Akihitimisha Kaimu mkuu wa chuo hicho Ndugu Lazaro Busagara Mbali na kushukuru kwa ujio wake kama mgeni rasmi amemuhakikishia kuwa chuo chake kitaendelea kuwa msaaada kwa Jamii inayokizunguka kwa kuanzisha miradi mbalimbali yenye kuinufaisha jamii hiyo huku akiomba kumalizwa kwa baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo barabara na usafiri jambo ambalo Mhe Dkt Angeline Mabula ameanza kulipatia majawabu

Sherehe  hizo pia zilihusisha zoezi la ugawaji wav yeti kwa walimu na wanafunzi kulingana na michango yao waliyoitoa wakiwa chuoni hapo

Mahafali ya Chuo hicho yanataraji kufanyika kesho siku ya Jumamosi Tareh 25.11.2017 yakitanguliwa na zoezi la harambee ya ujenzi wa mabweni ya wananfunzi wa chuo hicho

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
24.11.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com