Mjumbe wa mafunzo juu
ya mpango wa uendeshaji wa kijinsia Afisa wa Serikali za Mitaa Hussein
Mwatawala akipitia fomu zitakazotumika katika kukusanya taarifa za masuala ya
Kijinsia mkoani Singida.
Serikali kupitia Tume
ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeandaa Mpango wa uendeshaji wa
Kijinsia kwa ajili ya mwitikio wa Masuala ya Ukimwi ambao umetambulishwa rasmi kwa
timu ya Kuthibiti Ukimwi Mkoani Singida.
Mratibu wa Jinsia
Kutoka TACAIDS Jacob Kayombo ameongoza mafunzo hayo kwa timu ya kuthibiti
Ukimwi Mkoa wa Singida ambapo amewaeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuratibu
na kutoa dira katika utekelezaji wa program mbalimbali za Ukimwi kwa ngazi ya
Mkoa.
Kayombo amesema Mafunzo
hayo yamelenga kuutambulisha mpango huo pamoja na fomu zitakazotumika katika
ukusanyaji wa taarifa zihusuzo jinsia na Ukimwi.
“Mafunzo haya
tunayotoa yamejikita katika kuufafanua mpango huu utakavyotumika pamoja na
namna ambavyo fomu hizi zitatumika kukusanya taarifa za jinsia na Ukimwi kwa
Mkoa wa Singida na jinsi ambavyo taarifa hizo zitasaidia kufanya maamuzi sahihi
kuhusu masuala ya Ukimwi”, amesema Kayombo.
Ameongeza kuwa matarajio
yanayotegemewa baada ya mafunzo hayo kutolewa ni kuona masuala yote ya kijinsia
yanapewa kipaumbele katika program mbalimbali za Ukimwi.
Kayombo amesisitiza
kuwa mpango huu utakuwa ni mwongozo wa wadau wa masuala ya Ukimwi ili waweze
kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia usawa wa kijinsia hasa katika kuweka
mikakati ya kuthibiti Ukimwi yenye uelekeo wa Usawa wa kijinsia.
Amebainisha kuwa
mpango huu ambao umedumu katika kipindi cha mwaka 2016 mpaka 2018 una mwelekeo
mpya wa program za ukimwi wenye kuzingatia masuala ya kijinsia pamoja na
kuondoa changamoto zitokanazo na mila na desturi potofu za masuala ya kijinsia.
Naye Mjumbe wa
mafunzo hayo Afisa wa Serikali za Mitaa Hussein Mwatawala amesema mafunzo hayo
yametoa mwanga na mwelekeo utakawaosaidia katika kusimamia wadau wanaotekeleza
shughuliza Ukimwi ili wazingatie usawa wa kijinsia mkoani hapa.
Mwatawala amesema
maafisa waliopata mafunzo hayo wamepewa elimu ya kutosha juu ya mpango na wameufahamu
vema kazi iliyobaki ni kuhakikisha masuala ya usawa ya kijinsia yanapewa
kipaumbele katika kila program ya Ukimwi inayotekelezwa na wadau mkoani hapa.
Mpango wa uendeshaji
wa masuala ya Kijinsia 2016-2018 umeanzishwa kwa lengo la kutoa mwongozo kwa
wadau wa masuala ya Ukimwi ili watekeleze program zao katika mtazamo wa usawa
wa kijinsia.
Mpango huu
unashughulikia tofauti za kijinsia zikiwemo ukatili wa kijinsia, unyanyapaa na
ubaguzi ili kulinda haki za watu wote wakiwemo wanaume,wanawake,wasichana na
wavulana ili wapate huduma za uzuiaji wa maambukizi ya VVU, tiba, matunzo na
msaada.
Aidha mpango huu
unahusianishwa na Mkakati wa tatu wa taifa wa kuthibiti Ukimwi 2013-2018 na Mkakati
wa tatu wa kuthibiti VVU na Ukimwi wa Sekta ya Afya 2013-2017 ambapo mikakati
hiyo ina kanuni ambazo zinajumuisha usawa wa kijinsia na ulinzi wa haki za
binadamu.
0 comments:
Post a Comment