Leo Mapema M/kiti wa vijana wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini amekabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu za Mpira Wa Miguu kata ya Ndembezi,
M/kiti wa vijana wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Ndugu Dotto Joshua amekabidhi vifaa vya Michezo katika kata ya Ndembezi lengo likiwa ni Kuhakikisha anakuza Vipaji vya vijana katika wilaya ya Shinyanga Mjini .
Pamoja na mambo mengine M/kiti amewataka vijana kutumia Michezo kama sehemu ya kuwaingizia kipato badala ya kukaa vijiweni uku wakisubilia Serikali iwaletee Ajira na badala yake watumia vipaji vyao walivyopewa na Mwenyezi Mungu kujikwamua kiuchumi, Pia amewataka na vijana wengine katika kata zao kuanza Kubuni ni namna gani wanaweza kuanzisha ligi za Mpira na ameahidi ofisi yake itaendelea kutoa Ushilikiano kwa vijana wote wenye nia ya Dhati katika kujikwamua kiuchumi, leo mashindano yanaanza katika kata yenu na kata zingine naamini zitaiga mfano huo, Niwatakie mashindano mema na mashindano haya yawe ni Chachu ya kuibua vipaji katika kata yenu.
Mwisho
M/kiti alitoa Jezi na kuwatakia kila la heri vijana hao.
Imetolewa na
Ofisi ya uvccm
Wilaya ya Shinyanga Mjini.
0 comments:
Post a Comment