Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana na Mratibu wa Ofisi ya Ukaguzi
Kanda ya Kaskazini Ndg Juma Mwinyimkuu mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Ukaguzi
Kanda ya Kaskazini mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Kilimo Bi
Hilda Kinanga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Ukaguzi
Kanda ya Kaskazini kwa ziara ya kikazi.
Baadhi ya wafanyakazi Ofisi ya Ukaguzi
Kanda ya Kaskazini-Arusha wakifatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo kwa njia ya simu kwa watumishi waliopo Mjini Dodoma kuongeza ufanisi katika kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe (Katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na
Maendeleo Dkt. Hussein Mansoor (Kulia), Mratibu
wa Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini Ndg Juma Mwinyimkuu (Kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Kilimo Bi
Hilda Kinanga
wakiwasili Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini.
Na Mathias Canal, Arusha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Methew John Mtigumwe Ametoa mwezi mmoja kwa Mratibu Ofisi ya Ukaguzi
Kanda ya Kaskazini Ndg Juma Mwinyimkuu Kufatilia na kuwabaini baadhi ya watumishi
wanaochukua Rushwa.
Mhandisi Mtigumwe alitoa maelekezo
hayo wakati alipotembelea Kituo huduma ya afya ya mimea kilichopo katika Kijiji
cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha
Kituo hicho kinajihusisha na Ukaguzi
wa Mazao na Udhibiti wa ndege waharibifu, Viwavijeshi pamoja na huduma ya kutoa
vyeti vya usafi (Phtosanitary Certificate).
Mhandisi Mtigunmwe alisema kuwa
Rushwa imekuwa tatizo sugu katika kituo hicho hususani katika utoaji wa vibali
vya usafirishaji wa chakula kinyume na taratibu.
Aliwaasa watumishi hao kuacha haraka
Utendaji mbovu, kuacha kuchukua Rushwa kwenye mipaka ni lawama nyingi kutoka
kwa wananchi kwani kufanya hivyo wanaichafua wizara nzima ya kilimo.
lakini pia hakuna maabara na
hawajatoa taarifa kwa Katibu mkuu wa wizara ya kilimo
"Nakupa mwezi mmoja uwakamate
watu wote wanaochukua rushwa pia uandike barua ya kunitaarifu kuwa kuna uhitaji
wa maabara" Alisema Mhandisi Mtigumwe wakati wa kikao hicho
MWISHO
0 comments:
Post a Comment