Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua kiwanda kidogo cha uzalishaji wa kahawa katika Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili Ofisi hizo kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua namna Kahawa inavyohifadhiwa tayari kwa kuingia sokoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maelezo ya kitaalamu kuhusu mchakato mzima wa kupaki kahawa na soko lake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Ndg Primus Kimaryo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe alipotembelea chumba cha kuchotea Sampuli zinazopelekwa ambazo ni kilo 8 na kuchotea Gramu 300 kwa Loti.
Muonjaji katika Maabara ya Kahawa Bi Regina Mushi Daud akiendelea na majukumu yake katika maabara ya Kahawa.
Kaimu Mkurugenzi
Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Ndg Primus Kimaryo Kutoka Bodi ya Kahawa akielezea mbele ya Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe namna wanunuzi wanavyokabiliana katika ununuzi wa Kahawa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazo
Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa wakifatilia kikao kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe katika Ukumbi wa Bodi hiyo.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe.Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya Kahawa ambayo ni Taasisi ya serikali
iliyopewa jukumu la kusimamia sekta ya Kahawa nchini kuongeza ufanisi katika
uzalishaji wa Kahawa nchini kwani Kahawa ni miongoni mwa mazao ya
kipaumbele.
Mhandisi Mtigumwe ametoa Rai hiyo
wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Mara baada ya kutembelea
Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya
Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa Mwaka 2011 wadau
waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya Kahawa ambayo lengo
kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia Tani 80,000 Mwaka 2017 na Tani
100,000 Mwaka 2021 lengo ambalo halijafikia na bado uzalishaji ni mdogo hivyo
kuongeza uzalishaji linapaswa kuwa jambo la haraka iwezekanavyo.
Katibu Mkuu Alimuelekeza Kaimu
Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na uhamasishaji Masoko Primus Kimaryo Kufanya
Utafiti ili kubaini nini chanzo cha uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi
kutotunza vizuri kahawa yao, Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri
zinazotumika.
Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali
inajipanga kwa kampeni kubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kufahamu umuhimu
wa kulima kwa wingi mazao ya Chakula na Biashara ikiwemo zao la Kahawa.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo, Alisema
miongoni mwa sababu ambazo huchangia uzalishaji mdogo katika mazao mbalimbali
nchini huwa ni pamoja na Wananchi kuchanganya mazao wakati wa kupanda jambo
ambalo sio rafiki sana katika Kilimo, sambamba na Kutoacha nafasi kati ya mche
na mche.
Mhandisi Mtigumwe aliitaka Bodi ya
Kahawa Kufanya Utafiti wa maeneo ambayo Kahawa inastawi kwa wingi ili kuongeza
sehemu za kuzalisha Kahawa kufikia uzalishaji wa kiwango kikubwa tofauti na
ilivyo hivi sasa.
Hata hivyo amesema kuwa
atazishughulikia haraka iwezekanavyo Changamoto za Uzalishaji, Changamoto za
Ubora, Changamoto za Masoko sambamba na Changamoto za Sekta.
Majukumu ya Bodi ya Kahawa ni pamoja
na usimamizi wa sheria namba 23 ya marekebisho yake ya Mwaka 2009 na kanuni za
Kahawa 2013 sambamba na kuratibu Majukumu shirikishi (Shared Functions) Baina
ya serikali na wadau.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment