Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akihimiza jambo kwa uongozi wa Benki ya Kilimo.
Na Mwandishi wetu, Lindi
Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid
Mohamed ameiasa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB)
kuwezesha wakulima ili waweze kuchangamkia fursa za kuuza mazao ya
kilimo nje ya nchi ili kuwaongezea kipato wakulima hao.
Waziri
Hamad aliyasema hayo alipolitembelea Banda la TADB katika Viwanja vya
Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini
humo.
Mhe.
Hamad alisema kuwa Tanzania inapata fursa nyingi za masoko nje ya nchi
kwa mazao mbalimbali ikiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde
ikiwemo dengu na mbaazi zinazotakiwa sana nchini India
na Arabuni.
“Naiomba
Benki ya Kilimo kuwawezesha wakulima wanaolima kibiashara ili
kuchangamkia fursa za masoko kwa mazao ya kimkakati yakiwemo zao la
karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo dengu na mbaazi ambazo
nchi nyingi marafiki wanahitaji,” alisema Mhe. Hamad.
Aliongeza kuwa wizara yake inaletewa maombi mengi ya mazao kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nchi hizo.
Kwa
mujibu wa Waziri Hamad kuna wafanyabiashara wa kutoka Umoja wa Falme za
Kiarabu wanaohitaji zaidi ya kontena mbili za korosho kwa wiki hivyo
Benki ya Kilimo ina wajibu wa kuwezesha wakulima ili waweze
kuchangamkia fursa hizo.
“Naamini
Benki ikiwawezesha wakulima wanaweza kuchangamkia fursa za masoko ya
nje ikiwemo ya wafanyabiashara kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu
wanaohitaji zaidi ya kontena mbili za korosho kwa wiki,” aliongeza.
Akizungumza
wakati wa akipokea ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.
Francis Assenga alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa TADB ni kuchagiza
juhudi za serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa katika kutekeleza hayo Benki ya kilimo
imedhamiria na kujizatiti katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika
kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa
kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri
zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
“Lengo letu ni kuhakikisha tuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.
Ameongeza
kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta
hizo ili kuongeza tija sekta hizo ili kupambana na umaskini nchini.
0 comments:
Post a Comment