Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Shahada ya
Uzamivu katika Uchumi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck
Mwigulu Nchemba katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa
Rwekaza Mukandara.
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya
Uzamili Katika masuala ya Jiolojia wakifurahia mara baada ya kutunukiwa
rasmi shahada hiiyo katika Mahafali ya 47 ya chuo hicho leo Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye
pia alikuwa amidi wa shughuli za sherehe za chuo Kikuu cha Dar es
Salaam akimkabidhi mrithi wake Profesa Boniventure Rutinwa zana ya
kutumikikia nafasi hiyo wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho leo
Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara akitoa neno la shukrani mara baada
ya zoezi la kuwatunuku degree zao wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam leo jijini Dar es Salaam.
: Baadhi ya wahitimu wakiwa
katika nyuso za furaha kufuatia kuhitimu masomo yao kama walivyokutwa na
mpiga picha wetu katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
leo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba mara baada
walipokutana katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo
Jijini Dar es Salaam. Mwigulu Nchemba nimiongoni mwa wahitimu
waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Uchumi katika mahafali ya 47 ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Mlimani City.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Serikali waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu katika
Mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamala ya Usimaizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii
(SSRA) Dkt. Irene Isack. (Picha na MAELEZO)
0 comments:
Post a Comment