Kamishna Generali wa Idara ya
Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala, akizungumza jambo wakati
alipowasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Annarose Nyamubi
(Aliyeketi Katikati).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) Ndg.
Andrew W. Massawe akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea Kambi
ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana watakaoshiriki kuendesha zoezi
la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu akipokea
maelezo ya namna mafunzo yanavyotolewa kwa vijana wa JKT. Katikati ni
Afisa wa Nida mtaalamu wa mifumo ya komputa Bw Godfrey Surera ambaye
amekuwa akiendesha mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida
akisisitiza jambo mbele ya vijana wa JKT (Hawapo pichani) wakati
alipotembelea kambi ya Butiama kukagua mafunzo ya namna ya kutumia
mashine yanayoteolewa kwa vijana wa JKT. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Butiama Mhe. Mhe. Annarose Nyamubi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, viongozi wa
Kambi ya JKT Butiama na vijana ambao watashiriki kuendesha zoezi la
Usajili kwa wananchi wa Wilaya hiyo linalotarajiwa kuanza Jumatano
22/11/2017
………………………………………………………..
Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA), Ndg
Andrew W. Massawe amewasili rasmi mkoani Mara akiwa ameambatana na
Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter
Makakala tayari kwa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa zoezi la Usajili
Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Mkoa huo utakaofanywa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni.
Mara baada ya kuwasili viongozi
hao walipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima ambaye
aliwatambulisha kwa wananchi wa Bunda kabla ya kukutana na Mkuu wa
Wilaya ya Butiama Mhe. Annarose Nyamubi ambaye pamoja na kuwapa ripoti
ya maandalizi ya Usajili kwenye Wiilaya yake, walipata fursa kutembelea
Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana ambao wataendesha zoezi
hilo ndani ya siku 60.
Akizungumza na vijana katika
Kambi hiyo, ndg. Masssawe amewataka kuwa wazalendo na makini katika
zoezi wanalokwenda kulisimamia kwa kuhakikisha wanalifanya kwa uangalifu
na nidhamu ya hali ya juu kwa faida ya Taifa lao.
“ tunafarijika sana tunapoona
zoezi hili likiendeshwa na vijana wa JKT kwani mara zote wamekuwa
wakijitoa kufanya kazi nzuri yenye uzalendo wa kweli kwa Taifa lao;
ndiyo maana nawapongeza kwa dhati uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa kuamua
kusimamia zoezi hili na kuweka malengo ya utekelezaji, na sisi tunaahidi
kwenu hatutawaangusha” alisisitiza.
Uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa
mkoa wa Mara utafanyika Jumapili 19/11/2017 na unategemewa kuhudhuriwa
na viongozi wote wa Mkoa wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi,
Madiwani, watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, watumishi wa umma,
Viongozi wa Dini na Wananchi.
0 comments:
Post a Comment