Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo
(Mb) amesema jumla ya watumishi wa Sekta ya Afya wapatao 2058 wamekwisha pangiwa
vituo vya kazi kuanzia leo 06/11/2017 na taarifa zote zinapatikana kwenye
mtandao wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.
“Taarifa ya watumishi 2058
imekamilika na itarushwa kwenye mtandao wa OR TAMISEMI leo tarehe 6/11/2017
jioni, hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini
wanatakiwa kujiandaa kuwapokea watumishi hao ikiwemo kuwapatia stahiki zao”
Amewataka Wakurugenzi wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waajiri kuhakikisha wanachukua taarifa za
watumishi walioripoti na kuwaingiza kwenye Mfumo wa Mishahara na kuwapangia
katika maeneo ambayo ya uhitaji mkubwa ili kuboresha huduma za afya nchini.
Pia ameekeza watumishi
wanaopangiwa vituo, kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu
tangazo hili kutolewa.
Aidha, Waajiri wote watoe
taarifa juu ya kuripoti kwa watumishio haa wapya na vituo walivyopangiwa siku
14 baada ya kuripoti kwao.
0 comments:
Post a Comment