METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, March 10, 2017

Serikali yaonya kasi ya utoro shuleni

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mmanga Mjengo Mjawiri
 
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema wimbi la utoro kwa wanafunzi limeshika kasi kubwa ambapo jumla ya wanafunzi 1,000 hawakufanya mitihani ya mwisho kidato cha nne mwaka jana.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mmanga Mjengo Mjawiri alisema hayo wakati akizungumza na walimu wakuu, wazazi na wajumbe wa kamati za shule wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Alisema tatizo la utoro kwa wanafunzi ni kubwa sana kiasi ya wanafunzi kushindwa kufanya mitihani ya taifa kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.

Aliwataka wazazi kuhakikisha wanaratibu nyendo za masomo ya watoto wao ikiwemo kufuatilia na kuona wanafanya mitihani ya taifa na kupata matokeo yao.

Aidha, walimu wakuu wametakiwa kufanya tathmini kujua maendeleo ya wanafunzi wao pamoja na ufaulu na kuwasilisha mbele ya Wizara kila mwaka hatua ambayo itaiwezesha Wizara kujua matatizo yaliyopo.

Baadhi ya wazazi waliozungumza katika mkutano huo, waliitaka Wizara ya Elimu kuajiri walimu katika baadhi ya shule kufuatia upungufu wa walimu katika baadhi ya masomo yakiwemo ya sayansi.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com