METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, March 10, 2017

Wahamiaji 68 wawasili Somalia kutoka Marekani

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi
 
MKUU wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amewataka wanawake waache tabia ya kumjadili mtu (kusengenya) badala yake wafanye kazi ya ujasiriamali wakati huu.

Zambi aliyasema hayo alipozungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya kambi ya watu wasiojiweza na walemavu, zilizohudhuriwa na wanawake watumishi wa umma, taasisi za fedha, Jeshi la Polisi pamoja na Jukwaa la Uwezeshaji Uchumi wanawake mkoani humo.

Alisema kuna fursa nyingi za kuweza kujipatia kipato bila ya kumtegemea mume ikiwemo, kusindika mazao ya kilimo, ufuta, karanga, muhogo, korosho na masoko yake yapo ya uhakika.

Alieleza kuwa kuwapo ubunifu, ari ya kufanya kazi ndiyo inayoweza kumlinda mwanamke siyo kukaa kupoteza muda wote kumjadili mtu au lugha nyingine kumsengenya huko ni kupoteza muda.

“Wanawake mshirikiane mara kwa mara anayejua hili basi amfundishe mwenziwe ili kufikia malengo. Ila natoa tahadhari mara nyingi mkifanikiwa mnaanza kuwadharau waume zenu hiyo si tabia nzuri,’’ alisema zambi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji uchumi wanawake Mwamtumu Msangi, alisema lengo la jukwaa hilo ni kuwaunganisha wanawake kuwa kitu kimoja mkoani humo ili waweze kujikomboa na kuondokana na umasikini.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com