
Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi
Miss Tanzania wa Zamani Shose Sinare na kamishna mstaafu wa TRA ,Harry
Kitilya n Sioi Sumari wakiwa katika kizimba cha mahakama ya kimu mkazi
kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili

Kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya na Sioi Sumari
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania
katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA,
Harry Kitilya na wenzake umekamilika.
Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri
Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo
ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.
Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni
Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa
kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD
milioni sita.
Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi,
Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa
jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta liugha za ujanja
ujanja.
“Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu
yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi
haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndaniya
nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.
Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema
kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilina inaonyesha kesi
imepiga hatua kwa kiasi Fulani hivyo ameugiza upande wa jamuhuri ukija
tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.
Mbali na shtaka la utakatishaji wa
fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa
nyaraka za uongo na kughushi.
Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika
tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa
Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya
Uingereza.

aliyekuwa Miss Tanzania Shose Sinare akishuka katika ngazi za mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment