Halmshauri
ya wilaya ya Kilosa Morogoro imesimamisha mishahara ya walimu 15
waliohamishwa mwezi Machi bila kulipwa stahiki zao za uhamisho na
kupelekea walimu hao kugoma hatua inayodaiwa ni kushindwa kufuata sheria
za utumishi wa umma katika kudai.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti walimu wa shule tofauti, Rehema Mkway mwalimu shule
ya sekondari Masanze, Isaya Milimi mwalimu shule ya msingi Msimba
Kilosa, wamesema walimu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya
kuhamishwa bila kulipa stahiki zao na kuleta usumbufu na kuvunja morali
ya utendaji kazi na kuisababishia serikali madeni yasiyo na msingi.
Akizungumza
kwenye mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kilosa
Katibu wa Chama hicho Flora Malomele amesema pamoja na kupatikana
mafanikio kadhaa lakini walimu wanakabiliwa na changamoto ikiwemo
kutolipwa stahiki zao kwa wakati huku katibu wa tume ya walimu (TSC)
Daudi Mchilu akasisitizia watumishi kuzingatia maadili ya utumishi wa
umma.
Kwa
upande wake Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa Noel
Abeid akijibu madai ya walimu hao ameahidi kushughulikia suala hilo
kwani halmashauri inatafuta fedha na kuwaonya watumishi wa umma
kutojichukuliwa sheria mkononi pale wanapoona mwajiri ameenda kinyume
cha sheria badala yake wafuate sheria zilizopo.
0 comments:
Post a Comment