WAZIRI
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameendelea kusisitiza kuwa wananchi hawapaswi kununua damu kwani huduma
hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali zote.
Hayo
amezungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Benki ya
damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI
ambapo uliuzuliwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.
“Watanzania
wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa
huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani
inatoka kwa wananchi wenyewe” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika
kuchangia damu ili kuweza kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa
wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati sahihi bila ya usumbufu
wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa anayo furaha kutimiza miaka miwili
tangu kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kupiga hatua katika
sekta ya afya hasa katika kupunguza rufaa za nje na kuwa na utaalamu wa
matibabu ya kibingwa kama vile upandikizaji wa figo, vifaa vya usikivu(
Coclea Impant) na kutibu magonjwa ya moyo.
Kwa
upande wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem
amesema kuwa wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha shilingi Milioni
200 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza kusaidia
kuboresha sekta ya afya nchini.
“Mbali
na kiasi hicho cha fedha pia tumetoa Dola za Kimarekani 500 ili kuweza
kusaidia walemavu mbalimbali katika kulejesha hali zao za kawaida hapa
nchini” alisema Bw. Al-Najem.
Aidha
katika uzinduzi huo wa Benki ya damu Balozi Al-Najem alijitolea damu
unit moja ili kuweza kuchangia benki hiyo ya taasisi ya Mifupa MOI ili
kuweza kuhamasisjha na wananchi wengine waweze kuchangia damu kwa msaada
wa wagonjwa wengine.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula
alisema kuwa katika kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua
nchini waliamu kuanzisha kambi za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya
taasisi zingine za afya kuiga mfano huo.
“Tunataka
kuhamasisha matibabu ya kibingwa kufanyika nchini pamoja na uchangiaji
damu kwani damu hiyo haitatumika MOI peke yake bali hata kwenye Taasisi
zingne na vituo vya Afya nchini kote” alisema Dkt. Lwezimula.
Sambamba
na tukio hilo Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa
Wanawake (WOW) Afrika Mashariki walijitolea kuchangia damu ili kuweza
kusapoti benki hiyo kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya
damu.
“Tumehamasika
kuja kuchangia damu ili kuweza kutoa mfano kwa wanachi wengie waweze
kujitolea katika uchangiaji huu wa damu ili kujenga taifa lenye watu
wenye afya bora” alisema Mkurugenzi wa WOW Bw. Martin Gabone.
0 comments:
Post a Comment