Leo 28/11/2017 Diwani wa Kata ya Saranga Mh.Haroun Mdoe Yusuf ameapishwa ili kuanza majukumu yake rasmi kama diwani.Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo na kushuhudiwa na umati wa wananchi.
Akiongea kabla ya zoezi la kuapishwa Diwani Mdoe ,Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ambae pia ndie aliekuwa msimamizi wa uchaguzi katika kata ya Saranga alinukuu kanuni ndogo za kudumu za halmashauri kanuni namba 71 (a) kiapo cha kukubali wadhifa wa kuwa Diwani kinasema nanukuu; kila diwani kabla ya kushika wadhifa wake kama diwani na kabla ya mkutano wa kwanza wa halmashauri atakula kiapo kama ilivyoonyeshwa kwenye nyongeza ya kwanza ya kanuni za kudumu kitakachosimamiwa na hakimu mkazi au wakili wa wilaya.
Aidha alifafanua kuhusu vitendea kazi ambavyo amemkabidhi kama mwongozo katika utendaji wake ambavyo ni :
1)Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo alifafanua kuwa yote yatakayotekelezwa katika majukumu yake ni yale ambayo yameelekezwa katika Ilani ya CCM 2015-2020 ambayo ndio inatekelezwa na serikali ya awamu ya tano ambayo ipo madarakani na si vinginevyo; Alisema Mkurugenzi Kayombo
2) Kanuni ndogo za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na akifafanua kuhusu kanuni ndogo Mkurugenzi amesema kwa kutumia muongozo wa kanuni hizo atafanya maamuzi mbalimbali kwa kufuata sheria hizo.
3) Kanuni za kudumu za halmashauri za Manispaa ya Ubungo,ambayo ni muongozo katika utekelezaji wa masuala mbalimbali.
4) Kanuni za maadili za Madiwani,ambapo alisema anatakiwa kuzisoma na kuzielewa ili kujiepusha na kutenda vitendo visivyo vya kimaadili kwa mujibu wa sheria. Hivyo atatakiwa kuzisoma na kizielewa na kuzitumia ili kuepuka kutenda yasiyo ya maadili.
Aidha alisistiza kuwa Mh .Diwani anaapishwa ili aende kutekeleza majukumu yake mara moja na itapendeza aanze majukumu yake leo tarehe 28 Novemba ya kuwahudumia wananchi bila kupoteza muda.
Akimwambia kuhusu suala la ofisi alimkumbusha kuwa hiyo itakuwa changamoto yake ya kwanza kukabiliana nayo katika kufanya mchakato wa kutafuta ofisi kwani ofisi ya kata ya Saranga ilichomwa moto siku mbili kabla ya uchaguzi uliopelekea yeye kuibuka kidedea kwa kura za kishindo 6956 ambayo ni sawa na asilimia 67% ya kura zote zilizopigwa.
Mara baada ya Mkurugenzi kutoa maelekezo ya Mwanzo hakimu Mkazi wa wilaya. Mh Boniface alifanya zoezi la kumuapisha Mh.Haroun Mdoe Yusuf kwa mujibu wa sheria.
Kuapishwa kwa Mh.Diwani Haroun Mdoe Yusuf kumefuatia ushindi wa kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio katika kata ya Saranga uliofanyika 26/11 /2017 ambapo alipata kura 6956 sawa na asilimia 67% ya kura zilizopigwa.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO MANISPAA YA UBUNGO DSM
0 comments:
Post a Comment