Kipindi cha Tunakumbushana #SiUchochezi ni kipindi kipya cha kila wiki kinacholenga
kuibua na kuonyesha masuala mbalimbali katika jamii ambapo kitakuwa katika
mfumo wa sauti, picha mnato pamoja na picha jongefu (video).
Kipindi hiki kimejikita kukosoa, kuonya
na kusifia masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii yakiwemo ya
kiutendaji, kisiasa, kiuchumi pamoja na kijamii nchini Tanzania.
Kinaandaliwa na kurushwa na mitandao
ya kijamii ya Binagi Media Group (www.bmghabari.com) pamoja na mitandao mingime rafiki kote
nchini, lengo likiwa ni kuamsha ari ya kimaendeleo katika jamii.
Rai ni kwa wadau wote wapenda
maendeleo kuungana na BMG katika kuhakikisha kipindi hiki ambacho kimeanza
kuruka hewani kwa mara ya kwanza hii leo Novemba Mosi, 2017 kinaleta matokeo
chanya katika jamii.
Binagi Media Group
0757 43 26 94
Mwanza
#PamojaDaima!
0 comments:
Post a Comment