Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana
Francis Assenga nara baada ya kupitia Mchoro wa Ramani ya Mkakati wa
Kiuchumi wa ‘One Belt One Road’ mjini Hong Kong hivi karibuni kwenye
tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo
kupitia Mkakati huo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzainia (TADB)
Bwana Francis Assenga (Katikati) akiwa na viongozi mbali mbali mara
baada ya kumalizika kwa Kikao chake na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa
China Capital Fund Management (Hong Kong) Bwana James Wang (kushoto
kwake). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa First Shanghai Capital
Ltd Bwana Allen Wang; Mkurugenzi wa Landmark Investments Hong Kong na
Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Bunge la China Dr. Annie Wu Chung; Katibu
Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania
Bwana Joseph Kahama; na Mkurugenzi Mtendaji wa First Shanghai Capital
Ltd Bi. Fanny Lee.
Kikao kati ya
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya kutafuta
mitaji na uwekezaji ya Hong Kong iitwayo China Alpha Fund Management
(HK) kilichofanyika katika Jengo la Two Exchange Square mjini Hong Kong
hivi karibuni ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utafutaji
Mitaji na Uwekezaji ya Hong Kong Bwana James Wang (Katikati). TADB
iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bwana Francis Assenga (Mwenye
Shati la Bluu na Tai) na kushoto kwake ni Bwana Joseph Kahama ambaye ni
Katibu Mkuu wa China-Tanzania Friendship Promotion Association. Kushoto
wa Kwanza ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wawekezaji wa China Alpha
Fund Management (HK) Ltd Bi. Kandice Au.
Kaimu
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana Francis
Assenga mwenye tai nyekundu kulia kabisa akiwa kwenye picha ya pamoja
na Viongozi wa Benki ya China Hong Kong baada ya kumalizika kwa Kikao
chao mnamo tarehe 20 Oktoba 2017. Kulia kwa Bwana Assenga ni Meneja Mkuu
wa BOC Hong Kong Bwana Chan Man Stephen; Katibu Mkuu wa Taasisi ya
Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama; na Watendaji
wa Benki hiyo Bi. Yiu Oi Yin Doris, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Biashara
inayoshughulikia Taasisi za Fedha; na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa
Mahusiano na Mabenki, Bwana Wong Chee Him Steve, wakiwa Makao Makuu ya
Benki ya China mjini Hong Kong.
Bwana Francis
Assenga katikati mwenye suti ya khaki ambaye ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB akipanda miti katika Shule ya Sekondari ya China
Foundation mjini Hong Kong kuashiria kuunga mkono Mapinduzi ya Mkanda wa
Kijani (Green Belt Revolution) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 35 ya
shule hiyo ambapo Bwana Assenga alialikwa kama Mgeni Maalum wa Shule
hiyo. Wageni wengine Maalum waliotoka nchi mbali mbali ni pamoja na
Bwana Joseph Kahama ambaye aliyealikwa kama sehemu ya Jopo la Washauri
wa Shule hiyo kwa miaka takriban 8 sasa na Mkurugenzi Mtendaji wa Japan
International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki (Mwenye Suti
bila Tai Kulia kabisa) toka Tokyo, Japan na Mkurugenzi wa China Mfuko
wa Uhifadhi Mazingira na Maendeleo ya Mkanda wa Kijani Profesa Frederick
Charles Dubee (Mwenye Mvi na Tai katikati) toka Hienola, Finland.
Kaimu
Mkurigenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis Assenga (Kushoto)
akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary
School (CFSS) Bwana Au Kwong Wing, zawadi toka Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania wakati Bwana Assenga alipokaribishwa kama Mgeni Maalum
wa Shule kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Sekondari hiyo Mjini Hong
Kong hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliwahimiza wanafunzi
wa shule hiyo kuhifafhi mazingira na kujikita kwenye teknolojia mbali
mbali za kilimo cha kisasa.
Baadhi ya
Wageni Maalum toka nchi mbali mbali duniani walioalikwa kwenye
Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya China Foundation
Secondary School (CFSS) yaliyofanyika shuleni hapo njini Hong Kong hivi
karibuni. Wa Nne toka kushoto mwenye tai nyekundu ni Bwana Francis
Assenga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB).
Wawakilishi wa
Tanzania Bwana Francis Assenga (Kaimu Mkuruvenzi Mtendaji wa TADB) wa
pili toka kushoto na Bwana Joseph Kahama (Katibu Mkuu wa Taasisi ya
China-Tanzania Friendship Association) wakikabidhiwa Zawadi ya Utambuzi
wa mchango wao kwenye shughuli za kiuchumi, kilimo na huduma za jamii
kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya Jiji Hong Kong.
Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bwana Au Kwong Wing na Kukia kabisa ni
Mratibu wa Maadhimisho hayo (Mwene shati jeupe).
…………..
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania hivi karibuni ilipiga hodi mjini Hong
Kong kujadiliana na Taasisi mbali mbali za Hong Kong na China kuhusiana
na fursa za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mitaji na uwekezaji kwenye
Sekta ya Kilimo nchini Tanzania.
Katika
ziara hiyo iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa
Kairuki na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya
China na Tanzania Bwana Joseph Kahama, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB
Bwana Francis Assenga walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
makampuni na taasisi kadhaa zikiwamo Benki ya China; China Capital Fund
Management (Hong Kong); First Shanghai Capital Ltd; Mwakilishi wa
China Africa Industrial Forum Ndugu Wenbao Tan ambaye ni Naibu Katibu
Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha China.
Wengine
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation
Bwana Takashi Kawasaki na Mkurugenzi wa China Biodiversity Conservation
and Green Development Foundation Prof. Frederick Charles Dubee.
Miongoni
mwa yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni jinsi Tanzania inavyoweza
kunufaika na fursa zilizopo kwenye Mikakati ya ‘Silk Road Economic Belt
and the 21st-century Maritime Silk Road’, ujulikanao kama ‘One Belt and
One Road Initiative’ (OBOR) ambapo kwa mujibu wa Mkakati huo, Tanzania
ndio lango kuu la kuingilia Afrika kwa fursa hizo za kiuchumi na
kibiashara toka Asia ambapo Tanzania inakuwa kama kiungo muhimu hivyo
kuweza kunufaika zaidi ya nchi nyingine.
Miongoni
mwa fursa hizo ni pamoja na kukuza uwekezaji kwenye miundombinu ya aina
zote, viwanda vikubwa na vya kati, biashara kati ya Afrika na Asia, na
Huduma mbalimbali.
Aidha,
Bwana Assenga alikutana pia na akina mama wa shirika lisilo la
kiserikali la kukuza uchumi kwa akina mama wa Hong Kong wanamiliki pia
Shule ya Sekondari kama mchango wao kwenye huduma za jamii.
0 comments:
Post a Comment