Waziri wa nchi ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akisisitiza umuhimu wa Wakuu wa Mikoa
Kusimamia Kampeni ya uanzishwaji wa viwanda 100 katika kila Mkoa wakati
akizindua kamapeni hiyo leo Mjini Dodoma.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akizindua Mwongozo wa Kampeni ya
uanzishwaji wa Viwanda kwa kila Mkoa hapa nchini ili kuendana na dhana
ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisistiza ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akieleza umuhimu wa Ujenzi wa Viwanda katika kuzalisha ajira kwa
Vijana na kukuza uchumi wa nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akionesha moja ya viatu vinavyozalishwa hapa
nchini katika Viwanda vidogo na vya Kati wakati akikagua mabanda ya
wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo za ngozi mara
baada ya kuzindua kampeni yenye kauli Mbiu ya “Mkoa Wetu Viwanda vyetu”
ili kuhamasisha ujenzi wa Viwanda katika Mikoa yote nchini.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
baadhi ya Wakuu wa Mikoa(kushoto), kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya ujenzi wa
Viwanda vidogo na vya kati katika kila Mkoa.
( Picha zote na Frank Mvungi – Maelezo, Dodoma)
…………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda
vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini, leo
Mjini Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Mhe. Jafo amesema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili nchi iweze kuendelea
inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda.
“Historia ya Viwanda siyo ngeni
katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961 Serikali imekuwa
ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo tokea wakati huo
viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa na kusimamiwa huku
sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na Serikali” ameeleza Mhe.
Jafo.
Aidha amesema kuwa ili azma hiyo
iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa mwongozo wa
namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa
maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza
sekta hiyo nchini.
“TAMISEMI kupitia Mikoa na
Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu
ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa uanishe Viwanda
vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za Viwanda zinazopatikana
kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya soko” amefafanua Mhe.
Jafo.
Hata hivyo, Mhe. Jafo amewataka
Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na Halmashauri kuwatumia ipasavyo
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ugani ili kuwahamasisha wananchi
kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa
Wizara yake itaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na
kuanza kujenga majengo maalumu kwa ajili ya uendelezaji viwanda katika
Ofisi zote za SIDO Mikoani.
Naye Waziri wa Nchi ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama amesema kuwa Kauli Mbiu ya Mkoa wetu viwanda vyetu
itapunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini.
0 comments:
Post a Comment