METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 28, 2017

VITAMBULISHO VYA TAIFA KUWANUFAISHA WAFUGAJI WILAYA YA LONGIDO

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Godfrey Daniel Chongolo leo amekagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu lenye kulenga kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.Katika ziara hiyo Mhe. Chongolo amesema kwakuwa idadi kubwa ya wananchi wa Wilaya hiyo ni kutoka jamii ya Wafugaji; Kama Wilaya wamejipanga katika kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa vitakavyosaidia kuondokana na changamoto kubwa ya Wahamiaji Haramu; changamoto ambayo ni kubwa kutokana na kupakana na nchi nyingi jirani. Faida nyingine ni  kuwawezesha wananchi wake ambao niwa jamii ya wafugaji kufanya
shughuli zao kwa urahisi zaidi hasa wanapokuwa wakihama hama kutafuta malisho ya mifugo.“ Katika kuwasajili wananchi moja ya kikwazo kikubwa hapa ni elimu ya kujua kusoma na kuandika na lugha. Lakini kama Serikali tumejipanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii kwa kutumia wataalamu tulionao” alisisitiza.Wananchi katika Wilaya hiyo ambao asilimia kubwa ni wa jamii ya Maasai; wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali  kutoa Vitambulisho vya Taifa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata bughudha kubwa toka upande wa Kenya wanapokuwa malishoni kwakuwa wananchi wa Kenya tayari wanatumia Vitambulisho kuwatambua maarufu kama “Kipande”.Wilaya ya Longido inakisiwa kuwa na takribani wananchi 120,000 ambao watasajiliwa Vitambulisho vya Taifa, huku idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ikikadiwa kuwa zaidi ya asilimia 65%. Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Longido wakipigwa picha na mashine maalumu ya Usajili wakati zoezi hilo likiendelea Wilayani hapo. Hawa ni watendaji wa Vijiji vya Namanga na Longido wakichambua fomu za wananchi wao ili kutoa fursa ya kusajiliwa. Mhe. Godfrey Daniel Chongolo (Mwenye suti- kushoto) akikagua fomu za wananchi ambao wamesajiliwa kwa ajili ya kupigwa Picha na Saini ya Kielektroniki alipotembelea vituo vya Usajili Kata za Namanga na Karatu. Katikati ni Afisa Usajili Wilaya ya Longido Bw. Emmanuel Tarimo na Kulia ni Bw. Elisha Noel Afisa Usajili Msaidizi.Mhe. Chongolo akiangalia namna taarifa za mwananchi zinavyoingizwa kwenye mfumo kwa kutumia mashine maalumu (Mobile Enrollment Unit –MEU). Michuzi
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com