Mmoja wa wafanyakazi katika Wakala
wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA)
akitengeneza vigae vya kuezekea nyumba vilivyofanyiwa utafiti Jijini
Dar es Salaam tayari kwa matumizi ya ujenzi wa nyumba.
Ukuta unaofanyiwa utafiti kwa
ujenzi wa kutumia tofali mbichi kwa majengo makubwa na nyumba za makazi
ulioko katika karakana ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na
Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Jijini Dar es Salaam.
Mhandishi na fundi sanifu wa
majengo Bw.Hussein Mataka akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani ) kuhusu mashine ya kufyatua tofali iliyoko katika karakana la
ofisi hizo Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa ofisi za Wakala wa
Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Bw. Benedict
Chilla akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma
zinazotolewa na ofisi hiyo mapema wiki hii Jiji Dar es Salaam.
Mashine ya kupima ubora na kiwango
cha udongo kwa ujenzi wa nyumba ambayo ni moja ya vifaa bora
vinavyopatikana Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya
Ujenzi (NHBRA) kama inavyoonekana kwenye picha. Picha na Paschal Dotto-MAELEZO
Na. Paschal Dotto- MAELEZO.
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa
Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) imewashauri wananchi kufuata
maelekezo katika ujenzi wa nyumba za makazi na majengo mbalimbali ili
kupata nyumba bora.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam
Mhandisi Benedict Chila alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa utafiti
kwa nyumba za makazi kuhusu matumizi bora ya vifaa vya ujenzi kama
matofali, kokoto pomoja na mchanga uliobora katika ujenzi.
“kuna uhitaji mkubwa wa tafiti
ambazo zitawawezesha watanzania kupata makazi bora yenye kudumu, kwani
katika vifaa na huduma zinazopatikana kwetu zinajikita zaidi katika
usanifu majengo pamoja na matumizi ya vifaa, kwa hiyo tafiti hizi ni
muhimu kwa wananchi wenye mahitaji ya makazi bora”,.alisema Mhandisi
Chila.
Aidha Mhandisi Chila alisema kuwa
katika kutambua uhitaji wa wananchi NHBRA imetoa mlango kwa jamiii
kupata huduma bora kwa kufanya tafiti katika sanifu ya majengo na vifaa
vya kutumia katika ujenzi ili kupata makazi bora.
Kwa upande wake fundi sanifu wa
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba bora na vifaa vya ujenzi (NHBRA)
Bw. Hussein Mataka alisema kuwa wamejidhatiti katika kutoa huduma bora
kwa kufanya utafiti na kutoa bidhaa safi kwa ujenzi wa nyumba za makazi
na majengo mengine.
“Tunahitaji watanzania waje kwa
wingi na watambue uwepo wa bidhaa zetu kwani ni bora na zinatoa makazi
bora kwa sababu zimefanyiwa tafiti za kutosha na kutengenezwa katika
kiwango kizuri zaidi kwa matumizi ya muda mrefu”, .alisema Bw. Mataka
Akibainisha baadhi ya bidhaa hizo
Mataka alisema vifaa vinavyopatikana NHBRA ni matofali ya kufungamana
yanayotengenezwa kwa udongo na kiasi kidogo cha saruji, mashine za
kutengeneza matofai hayo, vigae vya kuezekea nyumba na mashine ya
kutengeneza vigae hivyo.
Mataka aliongeza kuwa tafiti
mbalimbali zinazoendelea kufanywa na NHBRA zina lengo la kupunguza
gharama za ujenzi wa makazi na majengo mengine ya biashara, alieleza
baadhi ya tafiti hizo ni utafiti wa kutengeneza frem za milango kwa
kutumia zege, utafiti kuhusu matofali yanayofungamana na kuchoma pamoja
na vigae vya kuchoma vya kuezekea.
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa
Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) ulianzishwa mwaka 2001chini ya
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kutoa huduma
na kupunguza gharama kwa vifaa vya ujenzi kwa makazi bora.
0 comments:
Post a Comment