Kufundisha Kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu
Walimu
ni msingi mkuu katika ustawi wa muda mrefu wa kila jamii kwa kuwa
hujishughulisha kuwapatia watoto, vijana na watu wazima elimu na ujuzi
wanaohitaji ili kufikia uwezo wao.
Lakini
duniani kote, walimu wengi sana hawana uhuru na msaada wanaohitaji
kufanya kazi yao iliyo muhimu sana. Ndiyo maana maudhui ya Siku ya
Walimu Duniani kwa mwaka huu – ‘’Kufundisha kwa Uhuru, Kuwawezesha
Walimu’’ – inathibitisha thamani ya walimu waliowezeshwa na kutambua
changamoto ambazo wengi hukabiliana nazo katika maisha yao ya kitaaluma
ulimwenguni kote.
Kuwa
mwalimu aliyewezeshwa ina maana ya kuwa na uwezo wa kupata mafunzo yenye
ubora, malipo ya haki, na fursa zisizo na mwisho za kujiendeleza
kitaaluma. Pia inamaanisha kuwa na uhuru wa kuunga mkono maendeleo ya
mitaala kitaifa – na uhuru wa kitaaluma wa kuchagua njia sahihi na mbinu
zinazofaa zaidi kuwezesha utoaji wa elimu yenye ufanisi, jumuishi na ya
usawa.
Zaidi ya hayo, inamaanisha kuwa na uwezo wa kufundisha kwa
usalama wakati wa mabadiliko ya kisiasa, machafuko, na migogoro.
Lakini
katika nchi nyingi, uhuru wa kitaaluma na uhuru wa mwalimu viko chini
ya shinikizo. Kwa mfano, katika ngazi za shule za msingi na za sekondari
katika baadhi ya nchi, mipango ya uwajibikaji imeweka shinikizo kubwa
kwa shule kutoa matokeo kwa vipimo vilivyowekwa, na kupuuza haja ya
kuhakikisha mtaala wa msingi unaofaa mahitaji tofauti tofauti ya
wanafunzi.
Uhuru
wa kitaaluma ni muhimu kwa walimu katika kila ngazi ya elimu, lakini ni
muhimu zaidi kwa walimu wa elimu ya juu, ili uwawezeshe kutumi uwezo
wao wa kuvumbua, kuchunguza, na kuendeleza utafiti kuhusiana na namnaza
kisasa zaidi za kufundisha. Katika ngazi ya elimu ya juu, mara nyingi
walimu hupatiwa mikataba ya ajira ya kipindi maalumu.
Hii inaweza
kusababisha hali ya kutokuwa na uhakika wa ajira kwa walimu, kupungua
kwa matarajio ya kukua kitaaluma, mzigo mkubwa wa kazi na malipo duni –
yote haya yanaweza kuzuia uhuru wa kitaaluma na kudhoofisha ubora wa
elimu ambayo walimu wanaweza kutoa.
Katika
ngazi zote za elimu, shinikizo la kisiasa na maslahi ya kibiashara
yanaweza kuzuia uwezo wa walimu kufundisha kwa uhuru.
Waalimu wanaoishi
na kufanya kazi katika nchi na jamii zilizoathiriwa na migogoro na
machafuko mara nyingi hukabiliwa na changamoto kubwa zaidi, ikiwa ni
pamoja na kupungua kwa kuvumiliana, ubaguzi, na vikwazo vinavyohusiana
na utafiti na kufundisha.
Mwaka
huu unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Mapendekezo ya UNESCO ya
1997 kuhusu Hali ya Wakufunzi wa Elimu ya Juu, ambayo inakamilisha
Mapendekezo ya UNESCO / ILO ya 1966 kuhusu Hali ya Walimu. Kwa pamoja,
vyombo hivi hufanya mfumo mkuu wa rejea juu ya haki na wajibu wa walimu
na waelimishaji. Yote yanasisitiza umuhimu wa uhuru wa mwalimu na uhuru
wa kitaaluma katika kujenga ulimwengu ambapo elimu na kujifunza ni kwa
ajili ya wote.
Wakati
dunia inapofanya kazi pamoja ili kufikia maono ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu, tunawaomba washirika wetu katika serikali, sekta ya elimu na
sekta binafsi kujitolea kubeba jukumu la kuwaandaa waelimishaji wenye
ujuzi ulio bora zaidi, wenye thamani na waliowezeshwa.
Hii ni njia
muhimu katika kuyafikia maono ya Malengo ya Maendeleo Endelevu hasa
lengo namba 4 lenye nia ya kuwa na ulimwengu ambapo kila msichana,
mvulana, mwanamke na mwanaume wanapata elimu bora na fursa za kujifunza
katika maisha yao yote.
Hii
inamaanisha kuwapatia walimu mazingira mazuri ya kazi na mishahara iliyo
bora, ikiwa ni pamoja na walimu wa ngazi ya juu. Inamaanisha kuwapa
walimu mafunzo na fursa ya kujiendeleza.
Inamaanisha kuongeza idadi ya
walimu wenye ubora, hasa katika nchi zenye idadi kubwa ya walimu na
waelimishaji wasio na elimu ya kutosha. Inamaanisha ya kuondoa vikwazo
visivyo vya lazima katika utafiti na kufundisha na kulinda uhuru wa
kitaaluma katika ngazi zote za elimu. Na mwisho, inamaanisha kuinua
hadhiya walimu duniani kote kwa namna ambayo inaheshimu na inayoonyesha
matokeo waliyonayo walimu katika jamii.
Katika
Siku hii ya Walimu Duniani, ungana nasi katika kuwawezesha walimu
kufundisha kwa uhuru ili kwamba, kila mtoto na kila mtu mzima awe huru
kujifunza – kwa manufaa ya dunia iliyo bora zaidi.
Imetolewa
na Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO; Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu
wa ILO; Anthony Lake, UNICEF Executive Director; Achim Steiner, UNDP
Administrator; pamoja na Fred van Leeuwen, General Secretary of
Education International.
0 comments:
Post a Comment