METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, October 8, 2017

SHAKA: "MCHWA" KWENYE HALMASHAURI WATEKETEZWE

"Serikali kuu imekuwa ikituma fedha nyingi  zisaidie uendeshaji miradi ya maendeleo kwenye ngazi za mitaa,  vitongoji, vijiji na kata badala yake huishia  mifukoni ya wajanja huku malengo ya Serikali yakikosa kufikiwa." - Shaka

"Hakuna njia mbadala ya kulifanya Taifa kujitegemea na kukuza maendeleo ya kisekta kama  elimu, maji, afya, mifugo , barabara,  uvuvi na kilimo ikiwa fedha zinazotengwa kwa shughuli hizo zinaibiwa." - Shaka

"Tumuunge mkono Rais Magufuli  katika dhima ya kuteketeza mchwa wala fedha za umma kwenye Halmashauri za wilaya. Tungependa kuona miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha za umma ikileta manufaa kama ilivyokusudiwa" -  Shaka 

"Msukomo pekee wa kisera katika kuboresha huduma za kijamii ni kuhakiksha mipango iliyopitishwa aidha na Bunge au Mabaraza ya Madiwani,  utekelezaji wake  uonekane aidha  kwa matumizi ya  thamani ya fedha na viwango vya  ubora." - Shaka

"Iwe ni  dhambi kwa fedha za umma kuibibwa  huku maelfu ya Wananachi wakikosa huduma za jamii ikiwemo ukosefu wa dawa, vifaa tiba, madarasa, barabara au majisafi na salama." - Shaka

"Kundi la Wafanyanyakazi ni kubwa si watumishi wa kwenye Halmashauri za wilaya peke yake. Wapo Wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi kwa upande mmoja pia ikumbukwe maskini vijijini hawapati umeme, zahanati na vituo vya afya zinahitaji  kuwa na dawa" - Shaka

"Wapo  Waganga , Wakunga, Wauguzi na Walimu wanaishi vijijini katika nyumba ambazo si bora pamoja na Wataalam wengine wa ugani. Iwe ni  haramu na mwiko mtumishi yeyote mwenye dhamana  kutumbua fedha za umma bila kuchukuliwa hatua za kisheria." - Shaka

"Rais hawezi kuzumgumzia mapema nyongeza ya mishahara kwa kundi moja la sekta ya umma  ili apigiwe makofi ya unafki wakati kuna wafanyakazi katika sekta binafsi  hawalipwi mishahara minono, haki na stahili zao bado wanapunjwa kinyume na jasho wanalolitoa." - Shaka

"Wapo Wahudumu wa ndani, Walinzi, Madereva, Wahudumu wa baa na hoteli bado wanalipwa ujira mdogo usiokidhi maisha yao hivyo kuliahidi kundi moja kwa matarajio yasio na manufaa ni kuyapuuza makundi mengine ya wafanyakazi." - Shaka

"Macho ya Wananchi ni Madiwani, ndio Watetezi na wapigania maslahi ya yao  kwenye Mitaa,  Vijiji na Vitongoji kila Diwani ajue anao wajibu kutetea maslahi ya wapiga kura wake atambue  ana haki kulinda fedha za umma." - Shaka 

"UVCCM tutaendelea  kumuunga mkono Rais Dk Magufuli na Serikali yake kwa nia ya kuwatetea wanyonge ili kila Mwananchi aishi kwa kuongozwa na  uzalendo, afanye kazi kwa bidii, azalishe na kujituma kupata riziki halali." - Shaka

Shaka Hamdu Shaka ni Kaimu Katibu Mkuu UVCCM aliyasema hayo Kipunguni Ilala jijini Dar es Salaam katika majumuisho ya ziara yake ya kutembelea kata ya Pugu na kipunguni kukagua miradi ya maendeleo ya Vijana pamoja na uhai wa chama na jumuiya zake.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com