METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, October 8, 2017

DC NDEJEMBI AZIDI KUBORESHA MIKAKATI YA KILIMO BORA WILAYANI KONGWA

Kongwa, Dodoma

Hii leo alikuwa na kikao kisha alizungumza na waandishi wa habari, alisema,  " Leo nimefanya kikao na watendaji wa kata zote za Kongwa, Maafisa Ugani wote wa Wilaya ya Kongwa na Idara ya Kilimo. Lengo la kikao ni kujipanga kwa msimu ujao wa Kilimo.

Msimu uliopita wa kilimo 16/17 tuliweka mkakati wa kilimo cha mtama (ONJAKO) na kufanikiwa kwa asilimia 113 (tulivuka lengo) na kutokua na njaa kabisa Wilayani Kongwa.

Msimu huu ujao 17/18 tunataka zalisha Mtama na Uwele zaidi ili wananchi waweze kuuza. Si rahisi kubadili watu walio zoea kulima mahindi, ila kwa hali ya mkoa wetu na uchache wa mvua ni lazima tuwabadili zaidi.

Tunataka soko kuu la mtama liwe Kongwa na wengine waje jifunza hapa kilimo cha mtama.  

Na tunayafanya haya kwa msingi mmoja tu wakuleta Maendeleo nakuboresha Maisha ya Watanzania  na huu wote ni msingi wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Vitendo, kwa kuzingatia sera ya Hapa Kazi Tu."

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com