METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, October 17, 2017

SERIKALI YA IRELAND YAWEKEZA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KUPAMBANA NA UKATILI WILAYANI MISUNGWI

Na G SengoBlog, Mwanza

SERIKALI ya Jamhuri ya Ireland kupitia Shirika la Maendeleo nchini humo limetoa msaada wa kiasi cha Uero 350,000 (zaidi ya milioni 700) kwa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwezesha mpango wa kujenga uwezo wa jamii na taasisi za Serikali ili kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata 10 wilayani Misungwi mkoani hapa.

Msaada huo umetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon,  aliye ambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo nchini humo, Ruairi De Burca pamoja na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock, kwenye uzinduzi wa Mradi wa mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi.

Kata zilizo nufaika na mradi huo ni pamoja na Usagara, Idetemya, Kolomije, Igokelo, Misungwi, Mbarika, Misasi, Nundulu, Sumbugu na Mabuki walengwa watakaofikiwa moja kwa moja  144,744 na wengine 289,488 ambao watafikiwa kwa kupata elimu kutoka kwa wananchi wengine waliopata mafunzo.

Mwanamke mmoja kati ya saba nchini Tanzania amebainika kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, hatua  ambayo inazidi kuchangia kupunguza nguvu kazi ya taifa.

Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Ireland, Bwana Cannon amesema kuwa serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali ikiwemo kupambana na vitendo vya Ukatili, Afya na Mfuko wa kusadia kaya masikini nchini (TASAF) ili kuleta mabadiliko katika Nyanja ya Uchumi. 

Zaidi ya asilimia 40 ya Wanawake nchini (Tanzania) wamebainika kukumbwa na vitendo vya ukatili, hali ambayo haiwakumbi wanawake pekee bali pia wanaume, nao wameripotiwa kukumbana na vitendo hivyo vya ukatili nazo takwimu zikishindikana kupatikana ipaswavyo kutokana na wanaume hao kuona kama ni suala la aibu na fedheha kuripoti kwamba wametendewa ukatili.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewaonya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili akisema kuwa serikali haitosita kuchukuwa hatua kali kwa wahalifu hao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kivulini, Yasini Ally amema Wilaya Misungwi ilikuwa ikikabiliwa kiwango cha kutisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake kunyanyaswa na waume zao ambapo wamepambana  kwa kila hali hatimaye sasa wanashuhudia vitendo hivyo kupungua kwa kasi.

Awali kabla ya kuzindua mradi huo wa Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto unaoendeshwa na KIVULINI Waziri huyo ameshuhudia uzinduzi wa Zoezi la Uhawilishaji fedha katika kijiji cha Misungwi pamoja na kutembelea kituo cha Afya cha Misasi ambapo ameahidi Serikali yake itaendelea kuchangia katika utatuzi wa changamoto zake.

Kwa mjibu wa takwimu za Mwaka 2015/ 2016 zinaonyesha kuwa, vitendo vya ukatili wa kinjisia nchini ni asilimia 58 kitendo ambacho kimetajwa kuwa kinachangia shughuli za maendeleo katika jamii kusuasua. 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com