Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika moja
ya ziara zake alizozifanya hivi karibuni Mjini Zanzibar
Na.
Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali imejenga
kuta na kupanda mikoko katika fukwe mbalimbali hapa nchini ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yalikuwa yakisababisha uhalibifu mkubwa
katika fukwe hizo.
Hayo yameelezwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba
wakati wa mahojiano katika kipindi cha "TUNATEKELEZA"
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1) kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika
kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu Tano.
“Tumeamua kutafuta
fedha ili kupanda mikoko na kujenga kuta ili kudhibiti fukwe kuliwa na bahari,”
alisema Makamba.
Aidha, amesema kuwa,
mabadiliko ya tabia ya nchi katika fukwe za bahari yamesababisha kupotea kwa maeneo ya kilimo kutokana na maji
ya bahari kuingia katika mashamba na kuharibu mashamba hayo ambayo mengi ni ya
mpunga.
Makamba amesema kuwa
ujenzi wa kuta na upandaji wa mikoko utasaidia kulinda mashamba hayo kutoingiliwa
na maji ya bahari pamoja na kuzilinda fukwe za bahari ambazo ni moja ya vivutio
vya utalii wa nchini.
“Bila kuhifadhi mazingira
hakuna utalii, uzuri na ubora wa fukwe unategemea fukwe hizo kutoliwa na maji
ya bahari” alifafanua Makamba.
Kwa upande wa
Muungano, Makamba amesema Wizara yake imefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali
zilizokuwa zikiwakabili wakazi wa bara na visiwani likiwemo suala la usafirishaji
wa magari kwa pande zote mbili.
“Kulikuwa na
malalamiko mengi juu ya kutotambulika kwa magari yanayotoka upande wa Bara
kutotambulika upande wa Visiwani, hivyo
hivyo kwa magari yanayosajiliwa upande wa Visiwani kutotambulika upande wa Bara. Tumelisimamia na
kutaka kulimaliza katika sheria mpya za usalama barabarani” alifafanua Makamba.
Makamba amesema,
makubaliano ya sheria hiyo mpya yameshafanyika na kamati za pamoja zaTanzania Bara
na Visiwani zimepitisha sheria hiyo.
0 comments:
Post a Comment