Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea 'kusota' rumande
katika kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Ponda
alijisalimisha jana Ijumaa kituoni hapo kuitikia wito wa kamanda wa
kanda hiyo, Lazaro Mambosasa aliyemtaka kuripoti ndani ya saa 72
akimtuhumu kutoa lugha za kichochezi.
Mara baada ya kuripoti jana, alifanyiwa mahojiano yaliyodumu siku nzima kisha polisi walikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake.
Akizungumza
na Mwananchi leo Jumamosi, Kamanda Mambosasa amesema atalizungumzia
suala hilo baadaye baada ya kupata taarifa za suala hilo.
Msemaji
wa jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba ameliambia Mwananchi kuwa
ukaguzi ulifanyika jana usiku nyumbani kwa Sheikh Ponda kisha
akarejeshwa kituoni.
"Suala la dhamana bado ni gumu,
lakini mawakili wetu wanasema wanalifanyia kazi na lolote linaweza
kutokea tumwombe tu," amesema Sheikh Katimba
Jana
Jumamosi, mmoja wa mawakili wa Ponda, Yahaya Njama amesema mteja wake
alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi za kuchochea watu waweze kufanya jambo
baya.
0 comments:
Post a Comment