Kikundi cha viongozi wa Ukambani
kimeitaka jumuiya hiyo kuachana na upinzani na badala yake wamuunge
mkono Rais Uhuru Kenyatta.
Wakizungumza katika nyakati
tofauti kwenye kaunti za Machakos na Makueni wakati wa msafara wa
wapigadebe wanaojiita Uhuru Express, wazee wa baraza la uongozi wa jamii
ya Wakamba na kikundi cha washirika wa Jubilee wametoa wito kwa
kiongozi wa chama cha Wiper ambaye ni mshirika wa Nasa Kalonzo Musyoka
kuungana na chama tawala.
Wazee hao wakiongozwa na
mwenyekiti wao Boniface Kilonzo walizungumza na waandishi wa habari
katika hoteli ya Machakos ambako mwenyekiti wa zamani wa Bodi ya Chuo
cha Mafunzo ya Madaktari, Philip Kaloki aliwaalika wanasiasa katika
kikao cha Kambu, Kibwezi Mashariki
Kilonzo alimsihi kiongozi wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga kusitisha maandamano anayotaka yafanyike nchi nzima akisema yanachochea ghasia.
“Maandamano
haya hayafanyiki kwa nia njema kwa sababu yanalenga kuzua vurugu na
uharibifu wa mali. Huu ni uhujumu uchumi na unaoweza kuadhibiwa
kisheria,” alisema.
Pia alisema uamuzi wa Raila
kujiondoa kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 hauna nia
njema. “Njia pekee ya kufikia uongozi katika nchi yetu ni kupitia
sanduku la kura. Kujiondoa kwa Raila kushiriki uchaguzi ni ishara kwamba
ushiriki wao ulikuwa wa kibinafsi na si kwa masilahi ya Wakenya,”
aliongeza.
Viongozi hao walisema jamii yao inapoteza
mengi kwa kusimama na upinzani. Mbunge wa zamani Kisoi Munyao alisema
ushirika wa Kalonzo na Raila haubebeki tena na ni hasara kwa jamii ya
Wakamba.
0 comments:
Post a Comment