Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo
amesema hana mpango wa kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini na
anachofanya sasa ni kutekeleza ahadi za Rais John Magufuli kutatua kero
za wananchi.
Akizungumza leo Jumamosi katika mkutano na
waandishi wa habari Gambo amesema wanaosambaza uvumi kuwa atagombea
ubunge Arusha ni wanasiasa ambao hawajiamini na wameshindwa kutatua kero
za wananchi.
"Kazi ambazo nafanya kwa kushirikiana na
wasaidizi wangu wakuu wa wilaya ni kutatua kero na tumeachana na mambo
ya kisiasa kutembea na flashi wafanye wao sisi tunachapa kazi," amesema
Amesema
ni ukweli uliowazi baadhi wabunge hawaonekani majimboni na hivyo
kuwaachia viongozi wa Serikali kufanya kazi ambazo zilipaswa kufanywa na
wabunge.
Akizungumzia tuhuma za kununuliwa madiwani wa Chadema ambazo zilitolewa na wabunge wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema, Gambo amesema anaamini hakuna masuala ya rushwa.
Gambo amesema madiwani ambao wamejiuzulu wameridhishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais Magufuli.
"Kuna
madiwani wameondoka wa Arusha, Monduli, Ngorongoro, Arumeru, Hai,
Iringa na maeneo mengine hawa wote wameridhishwa na utendaji wa Serikali
ya awamu ya tano," amesema
0 comments:
Post a Comment