Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akizungumza na
wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), alipofanya ziara ya siku moja
kutembelea ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia), akitoa maelezo kwa Mhe. Ndugulile.
Picha ya pamoja
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulileleo ametembelea
Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pamoja na mambo mengine amepata taarifa
yautendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi
vya maabara na kusemakuwa bajeti ya dawa inayotolewa na serikali iendane
na hali halisi ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya
maabara kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.
Naibu waziri huyo ambaye ni mara yake ya
kwanza kuitembelea MSD tangu ateuliwe kwenyenafasi hiyo, amesema
hatua ya serikali kuongeza bajeti ya dawa kuanzia
mwaka wa fedha uliopita na mwaka huu ina lengo la kupunguza gharama
ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wadawa muhimu kwenye vituo vyote vya
Afya vya umma ili kumpunguzia mwananchi gharama zamatibabu.
Kwa upande mwingine Mhe. Ndugulile
amewataka watendaji wa MSD kuwa na utaratibu wakuwatembelea wateja wao
ili kuboresha huduma zaidi baada ya kusikiliza maoni, malalamiko n
ahata ushauri wao.
Sambambana hilo amewaagiza MSD
kitengo cha huduma kwa watejakutembelea wateja wao na
kuhakikisha kitengo cha Manununuzi Maalumu
(SpecialProcurement) kinaongeza kasi kwenye manunuzi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwakutokana na hatua
ya MSD kuagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, bei ya dawana
vifaa tiba imekuwa nafuu kwa watumiaji na kueleza kuwa mpaka sasa
tayari MSD imetoamikataba kwa wazalishaji 104, ambapo 11 kati yao ni
kutoka ndani ya nchi.
Mikataba hiyo nikwa ajili ya dawa na
vifaa tiba takribani 700.Aidha, ameeleza kuwa kiutaratibu MSD hupeleka
dawa moja kwa moja vituoni mara nne kwamwaka, yaani kila baada ya miezi
mitatu, mpango wa MSD sasa hivi ni kufikisha dawa hizo kilabaada ya
miezi miwili kwa mwaka mzima.
Amesema hatua hiyo ya kupeleka dawa moja
kwamoja vituoni itapelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nyakati
zote vituoni, hasa maeneoya vijijini.
Naibu Waziri huyo ameipongeza MSD
kwa koboresha utendaji wake, hasa katika hatua
yakupunguza muda wa taratibu za ununuzi kutoka miezi
tisa hadi miezi sita kwa ajili yakukamilisha mchakato
mzima wa manunuzi, kwa kufuata sheria na taratibu za
ununuzi wa Umma.
Katika ziara hiyo, Mhe. Ndugulile
amepewa taarifa ya kitengo cha ufuatiliaji wamwenendo wa
kazi za kila siku za MSD, kijulikancho kama Strategic management office
(SMO)ambacho kiko chini ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu.
Amewapogenza watendaji wote wa MSDkwa
mabadiliko wanayofanya hasa kwa wateja wao na watanzania kwa
ujumla.Naibu Waziri huyo amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya
Bohari ya Dawa (MSD)tangu mwezi Septemba, 2012 hadi mwezi Julai, 2016.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
0 comments:
Post a Comment