Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(kulia) akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Miliki katika Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)
Bw.Hamed Abdallah kuhusu miradi ya ujenzi wa shirika inayoendelea katika
eneo la Kijichi,Temeke,Dar es salaam. Mhe.Mabula alikuwa akikagua
utendajiwa sekta ya ardhi katika ziara yake ya siku mbili Jijini Dar
es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Felix
Lyaniva(kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(kushoto)katika ofisi za Manispaa ya Temeke
kukagua utendaji wa shughuli za sekta ya ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(katikati) akizungumza na
watumishi wa sekta ya ardhi wa Manispaa ya Temeke mara baada ya kukagua
utendaji wa utoaji huduma za sekta hiyo ambapo aliwataka kuongeza juhudi
za ukusanyaji wa kodi za pango la ardhi. Kutoka kulia ni Mbunge wa
jimbo la Temeke Mhe.Abdalla Mtolea,na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Temeke Bw.Abdalla Chaurembo.kulia kwa Mhe.Mabula ni Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Bw.Felix Lyaniva na Meneja NHC Mkoa Bw.Isaya Mshamba.
Kamishina Msaidizi wa Ardhi Kanda
ya Dar es Salaam na Pwani Bw.Mathew Nhonge akijibu hoja zilizoibuliwa na
Madiwani wa kata mbalimbali za Manispaa ya Temeke wakati wa ziara ya
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula
alipotembelea kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Manispaa
hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bibi.Sofia
Mjema akimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe.Angelina Mabula alipomtembelea kukagua utendaji wa shughuli za
sekta ya ardhi wilayani humo.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(kulia) akiangalia utendaji kazi
wa mfumo mpya wa ukusanyaji kodi ya ardhi wakati wa ziara ya siku mbili
Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hati Msaidizi kutoka
Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Brenda Kuringe akijibu
swali kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala
wakati wa kikao katika ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula kukagua utendaji kazi wa sekta
ya ardhi katika Manispaa hiyo. Picha na Paschal Dotto –MAELEZO
………….
Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezitaka Manispaa na Halmashauri
nchini kuongeza juhudi katika ukasanyaji kodi ya ardhi hatua inayolenga
kuongeza tija ya maendeleo ya sekta hiyo.
Akizungumza katika ziara yake ya
siku mbili kwa Manispaa za Kinondoni, Temeke na Ilala katika Mkoa wa
Dar es Salaam Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula alisema kuwa sekta ya ardhi katika Manispaa na
halmashauri mbalimbali nchini itajiendesha kwa ukusanyaji kodi kwa
pango la ardhi kuwa mzuri katika Manispaa hizo.
Mabula alisema kuwa ukusanyaji
kodi kwa njia ya mfumo mpya uliofungwa kwenye Manispaa ni njia bora ya
kupata mapato na kuendeleza sekta ya ardhi, kwa hiyo watumishi wa idara
hiyo waweke juhudi za kudai kodi hiyo hasa kwa wadaiwa sugu ambao
wanadaiwa madeni makubwa ya pango la ardhi.
“Katika mfumo huu wa kodi na
nimeona baadhi ya takwimu kwa wateja wanaodaiwa, kati ya wateja 35,000
nimechukua wateja 100 wanaodaiwa kuanzia 5,000,000 na jumla yao ni
bilioni 13 kwa hiyo tukiweza kuwadai tutapata pesa nyingi tu”, alisema
Mabula.
Aidha Mabula alisema kuwa juhudi
za ukusanyaji kodi zimerahisishwa kwani mfumo huo mpya utawawezesha
watumishi katika idara ya ardhi kupata takwimu kwa urahisi na kuweza
kupata majina ya wadaiwa sugu.
Aliongeza kuwa Maafisa ardhi
hawana budi kutumia mfumo huo mpya kwa kuwa hauhitaji muda mwingi
kutafuta taarifa katika mafaili yaliyopo masijala kwa ajili ya kukagua
takwimu na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha makusanyo ya kodi ya
ardhi.
Akiwa katika Manispaa ya Ilala,
Mabula aliwataka watumishi wa manispaa hiyo kuwa na umoja baina yao na
baraza la madiwani wa baraza la manispaa hiyo ili kuweza kushirikiana na
kuongeza juhudi za ukusanyaji mapato.
Aidha katika ziara hiyo Mabula
aliwataka Wakuu wa Wilaya kutoa taarifa kwa Serikali iwapo kutakuwa na
uhaba wa watumishi hususani katika maeneo yenye uhitaji mkubwa na Wizara
iangalie namna ya kuwapa watumishi na kurahisiha utendaji kazi.
0 comments:
Post a Comment