……………
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Isack Kamwelwe ametembelea Mradi wa Maji Longido, mkoani Arusha
kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wake, kwa lengo la kuhakikisha
unakamilika kwa wakati na kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Longido.
Mhandisi Kamwelwe ametembelea
mradi huo na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa, ambao Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi mnamo Oktoba 21, 2017 na
kuagiza ukamilike kwa wakati na kuanza kuhudumia wakazi wa Mji wa
Longido na Kijiji cha Engikaret.
‘‘Serikali imedhamiria kukabiliana
na changamoto ya upatikanaji wa majisafi na salama Wilayani Longido kwa
kutekeleza mradi huu mkubwa wa maji kutoka katika chanzo cha maji cha
Mto Simba kilichopo Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro umbali wa
kilomita 64 mpaka Longido.’’
‘‘Nimeridhishwa na hatua ya
utekelezaji wa mradi huu unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira ya Mji wa Arusha (AUWSA) na utaigharimu Serikali kiasi cha
Sh. bilioni 15.8 ambazo ni fedha za ndani’’, alisema Waziri Kamwelwe.
Mradi huo unategemea kuzalisha
lita 2,160,000 kwa siku wakati mahitaji halisi kwa sasa ni lita
1,462,000, na unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 100
(sawa na wakazi 26,145 kwa sasa) wa Mji wa Longido kufikia 2024 na
Kijiji cha Engikaret chenye wakazi wapatao 1,294.
0 comments:
Post a Comment