METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, July 17, 2019

WATEJA WATANO WA TIGO KUSHUHUDIA FAINALI ZA AFCON NCHINI MISRI

 Meneja Mawasiliano wa Tigo , Woinde Shisael (Kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza washindi 5 wa tiketi za kwenda kushuhudia mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri kupitia promosheni ya SOKA LA AFRICA inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, (Kushoto) Mtaalamu wa Huduma za ziada kutoka kampuni hiyo, Ikunda Ngowi.
 Mmoja wa washindi wa tiketi ya ndege kwenda nchini Misri kupitia promosheni ya SOKA LA AFRICA inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Lukundo Samuel Sikombe, kutoka mkoani Arusha akipokea stakabadhi ya kusafiria (boarding pass), kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Tigo , Woinde Shisael (kulia) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washindi wa tiketi ya ndege kwenda nchini Misri kupitia promosheni ya SOKA LA AFRICA inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Lukundo Samuel Sikombe, kutoka mkoani Arusha, akipokea stakabadhi ya kusafiria (boarding pass), kwa niaba ya washindi wenzake (waliosimama nyuma) kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Tigo , Woinde Shisael (kulia) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. --- Baada ya kuwezesha wateja wake watano kushuhudia mechi za ufunguzi za michuano ya mataifa ya Afrika, kupitia promosheni yake inayoendelea ya SOKA LA AFRIKA, leo Tigo imetangaza washindi wengine watano watakaogharamiwa safari za kwenda Misri kushuhudia mechi za fainali mubashara. Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, amewataja washindi hao watano ambao sasa wanakamilisha idadi ya washindi kumi wa promosheni hiyo kuwa ni Kaunda John Petro, kutoka Zanzibar, Mohabe Noah Senso, (Dar es Salaam), Jafari Abdallah Zitto, (Tanga), Shabani Msafiri James (Dar es Salaam), na Lukundo Samuel Sikombe, (Arusha). “Tigo, tunayo furaha kuona promosheni hii ya SOKA LA AFRIKA inawezesha wateja wetu wengine kujishindia safari ya kwenda kuona mechi za fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika sambamba na kuwezesha wateja kujishindia fedha taslimu kwa siku,wiki na kwa mwezi kuanzia laki moja hadi milioni 10.Vilevile tumefanikisha dhamira yetu ya kuwashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zetu”,alisema Shisael. Kupitia promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu washiriki wataendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu kila siku, kwa wiki na kwa mwezi. Ili kushiriki kinachotakiwa ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15670 au tembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz na kujibu maswali kuhusiana na michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri. Mashindano ya promosheni ya SOKA LA AFRIKA ni sehemu ya jitihada za Kampuni ya Tigo kuwashukuru wateja wake kwa kutumia bidhaa na huduma za Kampuni. Pia promosheni hii ni sehemu ya ubunifu ambao umelenga kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wateja.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com