Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na
Diwani wa viti maalum, Jesca Kalalio wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita ambapo pamoja na mambo
mengine Mhe, Kanyasu aliwaeleza wananchi hao kuhusiana na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na Serikali za kutafuta soko zuri kwa ajili ya
zao la pamba
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kasamwa waliokusanyika katika eneo la mkutano kwa ajili ya kumpokea Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini
Mhe.Constantine Kanyasu mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza
nan wananchi kwenye mkutano wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
katika eneo la Kasamwa mkoani Geita ambapo amewashauri wakulima wasiuze
pamba yao kwa walanguzi ambao wamekuwa wakinunua kwa bei ndogo.
Wananchi wa Kata ya Kasamwa wakimsiliza Mbunge wao, Mhe.
Constantine Kanyasu wakati wa mkutano uliofanyika mkoani Geita ambapo
amewataka kuwa wavumilivu huku Serikali ikiendelea kuwatafutia soko la
zao la pamba.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita, Bw. Barnabas Mapande
akizungumza na wananchi wa Kata ya Kasamwa kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini
Mhe.Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza nao.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu (katikati)
akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na watumishi wa Umma mara
baada ya mkutano wa hadhara kufunguliwa katia kata ya Kaswama mkoani
Geita.
Diwani wa Kata ya Kanyala, Mhe. Logaloga
akizungumza na wananchi kwa jinsi anavyoshirikiana na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine
Kanyasu katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Geita mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu
akiwatambulisha Makatibu wake kwa wananchi wa Kata ya Kasamwa mara baada
ya kuzungumza na wananchi hao mamabp mbalimbali ikiwemo bei ya pamba,
ufumbuzi wa suala la maji na nishati ya umeme
……………………….
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
amewashauri Wakulima wa zao la pamba wawe wavumilivu badala ya kuuza
pamba hiyo kwa walanguzi kwa bei ya chini huku Serikali ikiendelea
kuwatafutia soko zuri.
Amesema Serikali ilishaahidi kuwa kama
pamba hiyo haitanunuliwa kwa bei elekezi ya kilo moja kwa shilingi 800
hadi mwezi Agosti mwaka huu basi Serikali itainunua pamba hiyo ili
kuwafidia wakulima hao.
Hatua hiyo inakuja kufuatia
Wafanyabiashara wengi kushindwa kununua kwa bei hiyo kutokana bei ya
soko la pamba duniani kuporoka.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika
katika eneo la Kasamwa mkoani Geita, Mhe.Kanyasu amesema
wafanyabiashara wameshindwa kukopa pesa benki kwa ajili ya kuinunua
pamba hiyo kutokana na kukosekana kwa soko la kuiuza.
Mhe.Kanyasu amesema kufuatia hali hiyo
baadhi ya wakulima wamekuwa wakiiuza pamba hiyo kwa shilingi 500 kwa
kilo moja kwa walanguzi hali inayowadidimiza kiuchumi.
Ametaja mikakati ambayo tayari Serikali
imeshaichukua ikiwemo kuzungumza na Serikali ya Vietnam ambao tayari
wameonesha nia ya kununua pamba hiyo kwa Wakulima.
Aidha, Mhe Kanyasu amewaeleza Wakulima
hao kuwa Waziri wa Kilimo anatambua tatizo hilo na ameahidi kutembelea
mkoa huo kwa ajili ya kuzungumza na Wakulima hao.
Naye Juma Kaludushi ambaye ni mkulima wa
zao pamba amesema wakulima walio wengi akiwemo na yeye wamekuwa wakiuza
pamba hiyo kwa walanguzi kwa bei ya chini kwa hofu kuwa pamba hiyo
itaharibika mikononi mwao.
“Pamba ipo majumbani mwetu muda unakwenda
bora tuuze tu kwa Walanguzi ili isiharibike kuliko tukapata hasara
kabisa” Amesema Mkulima huyo.
Kwa upande wake, Ester Nalamo, ambaye ni
Mkulima wa pamba amesema amelazimika kuuza pamba kwa bei ya chini ili
aweze kuwalipia ada watoto wake kwa vile yeye hana chanzo kingine cha
mapato zaidi ya kuuza pamba.
0 comments:
Post a Comment