
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera anatarajia kuwa mgeni rasmi katikauzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tumaini Msowoya, katika ukumbi wa Highland Hall mjini Iringa.
Wageni wengine wa heshima kwenye uzinduzi huo
ni Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mkuu wa
Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki
cha Ruaha Baby Baraka Chuma, wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.
Akizungumza na Mwanaspoti, Msowoya alisema tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.
“Naenda
Iringa kurudisha shukrani zangu kwao, nataka wajue nipo huku sio tu kwa
sababu ya kazi bali huduma ya kuimba niliyoanza ”
Alizitaja
nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni Hakuna Matata, Mwamba,
Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu, Wanawake Jeshi Kubwa, Samehe na
Mungu wa Rehema.
“Kazi
hii nimeifanya chini ya usimamizi wa JB Production ikisimamiwa na
Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye meneja anayesimamia kazi zangu kwa
sasa,’ alisema Msowoya.
Wasanii watakaomsindikiza
Meneja
wa Msowoya, Smart Bilionea Producer Baraka alisema tayari waimbaji na
kwaya mbalimbali kutoka Iringa na Dar es Salaam watamsindikiza kwenye uzinduzihuo.
Alizitaja
kwaya zizothibitisha kumsindikiza kuwa ni Wakorinto wa Pili kutoka
Mufindi, Muhimidini na kwaya ya Vijana kutoka Iringa mjini.
Baadhi
ya waimbaji ni Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu ni
Mungu tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine
maarufu kwa jina la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses
Simkoko, Ritha Komba na Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.
Wengine
ni Rebecca Baraka, Jesca Msigwa, Ester Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis
Lukosi, Wadi Mbelwa, Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu Mgogo, Emma
Sanga na Victoria Mwenda kutoka Iringa.
“Waimbaji
watakaomsindikiza ni wengi nab ado tunaendelea kuwasajili wengine. Bado
tupo kwenye mazungumzo na Bahati Bukiku ambaye anaangalia ratiba yake,
ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.
Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya kutokana na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.
Historia
Hakuna Matata ni albamu ya pili ya Msowoya baada ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.
“Bahati
mbaya niliitengeneza kutokana na kiwango kidogo hivyo iliishia
kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii ni nzuri na wakazi wa
Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.
0 comments:
Post a Comment