Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyesimama
akiongea na wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga pamoja na wadau mbalimbali
wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa
Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi
na wakunga Bukumbi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kulia akipata
maelekezo kuhusu uuguzi na ukunga kutoka kwa mfanyakazi wa Chama cha
Uuguzi na Ukunga Bw. Stephano Simba kushoto alipotembelea banda lao
wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini
Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia
akikata utepe baadhi ya vitabu kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa
Ukunga salama wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Mwanza
katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi wa tatu kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda.
Mkurugenzi wa mradi wa Ukunga
salama Dkt. Julius Masanika akiongea na wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga
pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati
wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza
katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na
Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi Bi. Rose Julius
ambaye anafadhiliwa na mradi huo mahitaji yake ikiwamo pamoja na ada
wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini
Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi .
Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi na ukunga
SCIMVE Bw. Yohana Ngwandu akiongea na wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga
pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati
wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza
katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga
pamoja wakimsikiliza kwa amkini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani
wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini
Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Baadhi ya Wasanii wa Kikundi cha
sanaa Cha wakiigiza mama mjamzito anaelekea kituo cha kutolea huduma ya
afya mapema kwa ajili ya kujifungua salama wakati wa uzinduzi wa mradi
wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha
wauguzi na wakunga Bukumbi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto
akikabidhi matunda kwa baadhi ya wazee alipotembelea kambi ya wazee
Bukumbi jijini mwanza.
………………….
NA WAMJW-MWANZA
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa wadau
wa sekta ya afya na watoa huduma za afya hasa wauguzi na wakunga
wanatakiwa kujikita zaidi kwenye kuokoa na kuboresha afya ya mama
mjamzito na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza hayo wakati wa
uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama (More and Better Midwives)
uliofanyika leo katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi kilichopo
Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
“Sisi sote tunafahamu umuhimu wa
wauguzi na wakunga katika kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo
Serikali ya awamu ya tano tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa
kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa
Serikali inafahamu kuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada
mbalimbali za afya pamoja na nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi
ikiwa kutoa kipaumbele cha ajira za wauguzi na wakunga.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile
amewaonya wakunga na wauguzi wenye tabia ya kutumia lugha chafu kwa
wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo
inaendeshwa kwa taaluma na maadili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Misungwi Bw. Juma Sweda amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wanatakiwa
wawe mstari wa mbele katika kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa
gharama nyingi pindi wanapopata maradhi na mpaka hivi sasa wananchi
wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga
Salama nchini Dkt. Julius Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili
wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya
Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa kuwalipia ada pamoja na mahitaji
mengine.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa
Uuguzi na Ukunga katika Chuo cha Bukumbi ambaye anafadhiliwa na mradi
huo Rose Julius amesema kuwa anawasihi wanafunzi wafanye bidii kwenye
masomo ya sayansi na hatimae wachukue fani ya uuguzi na ukunga katika
kukabiliana na changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali na ufunguzi huo wa mradi wa
Ukunga salama unaojulikana kama “More and Better Midwives” ambao
umeshirikisha taasisi isiyo ya Kiserikali JHPIEGO ,wawakilishi kutoka
Chama cha wakungwa Canada(CMA) na Chama cha wakungwa Tanzania TAMA pia
alitembelea Zahanati ya Kambi ya wazee Bukumbi,Bohari ya Dawa (MSD) na
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure ili kujua hali ya
upatikanaji wa dawa .
0 comments:
Post a Comment