Na mwandishi wetu, Njombe
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imesema imejipanga katika kusaidia kuchagiza
kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini kwa wakulima mkoani Njombe na Tanzania kwa ujumla.
Ahadi imetolewa na
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rehema Twalib wakati alipouongoza
ujumbe wa Benki walipomtembelea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa
Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka mkoani Njombe.
Bibi Twalib alisema kuwa TADB ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kuunga mkono
juhudi za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania ili kuisaidia Serikali kuharakisha maendeleo ya sekta
ya kilimo ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya
asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
Aliongeza
kuwa Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na
kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta
mapinduzi katika
kilimo nchini.
“Katika kuhakikisha tunafikia malengo ya Serikali Benki imedhamiria
na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika
kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa
kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri
zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini” alisema.
Akizungumza na ugeni huo, Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe.
Christopher Ole Sendeka alisema kuwa ujio wa Benki hiyo mkoani Njombe
kutahamasisha shughuli za kilimo mkoani humo hali itakayochochea
maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani Njombe.
Kwa
mujibu wa Mhe. Ole Sendeka, mkoa wa Njombe umejaaliwa rasilimali nyingi
kwenye sekta ya kilimo ila changamoto za ufinyu mkubwa wa upatikanaji
wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo zinarudisha
nyuma juhudi za wakulima mkoani humo.
“Naishukuru Serikali kwa kuianzisha TADB kwani hali
ya ukosefu wa mitaji ya uhakika
inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha
kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kuwasahau
wakulima na wasindikaji wa mazao, hivyo tunaamini TADB itasaidia kutatua
changamoto hii,” alisema.
Bw.
Ole Sendeka alitoa wito wa wakulima mkoani humo kuchangamkia fursa hizo
za mikopo ya gharama nafuu inayotolewa na Benki ya Kilimo ili waweze
kuongeza uzalishaji na hivyo kujihakikisha kipato cha uhakika.
Kwa
upande wake, Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw.
Dickson Pangamawe alisema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo
ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati
(Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi
ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
Kwa mujibu wa Bw. Pangamawe mikopo hiyo ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na
kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
“Dhima
ya Benki yetu ni kuhakikisha tunawezesha maendeleo na kufanikisha
mapinduzi ya sekta
ya kilimo kwa kutoa mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwenye
miradi ya kilimo Tanzania inayolenga kukuza uchumi, kuhakikisha usalama
wa chakula na kupunguza umasikini wa kipato,” alisema.
0 comments:
Post a Comment